Abiria zaidi ya 100 waliokuwa wakitumia kivuko cha MV Nyerere kutoka Ukara kwenda Bugorora wamekwama kwenye maji ya Ziwa Victoria baada ya kutokea hitilafu kwenye Injini ya kivuko hicho na kuzimika.
Mbunge wa Ukerewe, Mheshimiwa JOSEPH MKUNDI ni miongoni mwa abiria waliokwama majini baada ya kuzima Injini ya kivuko hicho ameiambia Radio One kwamba abiria wamekwama kwa zaidi ya saa mbili.
Kuzima ghafla kwa kivuko hicho kilichokuwa na abiria pamoja na magari kunaleta wasi wsi kwa abiria na watu wa neo hilo.
Mbunge huyo wa Ukerewe amesem tatizo la kuvuko hicho amelieleza mara nyingi kwa mamlaka husika na wataalam wanasema kinahitaji kuwekwa Injini mpya ili kifanye kazi ipasavyo.
Habari za hivi karibuni zinasema abiria waliokwama kwenye kivuko hicho hatimaye wamefika salama Bugorora baada ya boti kadhaa kwenda kukivuta kivuko hicho hadi band
No comments: