MBUNGE
WA CHADEMA AACHIWA KWA DHAMANA YA SHILINGI MILIONI 10
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana baada ya
kusota rumande kwa siku sita.
Mdee ameachiwa leo Julai 10, kwa dhamana ya Sh10 milioni na
wadhamini wawili, baada ya kusomewa shitaka la kutumia lugha chafu na Hakimu
Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Mbunge huyo, alikamatwa Julai 4 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Ali Hapi aliyeamuru awekwe mahabusu kwa saa 48.
Hapi alidai, Mdee amemkashifu Rais na ndicho chanzo cha
kutupwa rumande kwa saa hizo.
Wakili Katuga amedai kwamba, mnamo July 3, mwaka huu katika
Ofisi za CHADEMA makao makuu, alimtukana Rais Magufuli kwa kumwambia anaongea
ovyo ovyo, anatakiwa afunge break.
Baaada ya kusomewa shtaka hilo Halima Mdee alikana kosa hilo
na kesi imeahirishwa kutokana na upelelezi kutokamilika mpaka tarehe 7 mwezi wa
8 mwaka huu ambapo kesi itatajwa tena.
No comments: