Rais taasisi isiyo ya serikali ya wanawake wenye mafanikio
Tanzania (Tanzania Women of Achievement….TWA) Irene Kiwia (Kulia) akiongea na
hadhara wakati wa kuzindua zana ya taasisi hiyo itakayotumika kiubunifu
kufundisha wasichana na wanawake nchini, uzinduzi huo umefanyika sambamba na
mkutano wa taasisi ya Graca Machel Trust unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Tarehe 09 Augst 2017, Dar es salaam, Tanzania: Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWA), leo
wamezindua jukwaa la kidijitali la kutoa mwongozo, ushauri na kujifunza kwa
ajili ya wasichana na wanawake Afrika ambalo linapatikana kwenye mtandao na
application ya simu lijulikanalo kama Twaa.
Jukwaa la ushauri la Twaa ni matokeo ya kazi endelevu za
taasisi ya TWA katika programu za
kujengea uwezo wanawake na wasichana zilizoanza mwaka 2009, zikiwa na malengo
ya kuboresha maisha, kukuza fursa na kusaidia wanawake nchini Tanzania
kufanikiwa ambao mwishoe watasaidia katika maendeleo ya jamii, nchi na bara kwa
ujumla.
Jukwaa hili limeandaliwa kwa ajili ya kuunganisha,
kukutanisha na kuwajengea uwezo wasichana kwa kuwawezesha kuchagua washauri
kutoka katika orodha kubwa ya wanawake wenye ujuzi katika nyanja mbalimbali; na
kujifunza masomo yaliyoandaliwa kwa ajili ya wasichana wa karne ya 21 katika
nyanja za Afya, Ubunifu, Maendeleo ya Biashara, Maendeleo Binafsi, afya ya
uzazi, haki, fasheni, urembo na mengine mengi.
Jukwaa la Twaa lina vijengea uwezo vingi ikiwa ni pamoja na
kutoa msaada wa ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa saikolojia, kuweka
mipango na utaratibu wa kutekeleza majukumu ili kuwasaidia wasichana kuweka na
kutimiza malengo yao kimkakati zaidi pamoja na kuwapa nafasi wasichana kuelezea
kazi zao na kuhamasishana wao kwa wao.
Akiongea katika uzinduzi uliofanyika sambamba na kongamano la
Women Advancing Africa lililoandaliwa na Graca Machel Trust jijni Dar es
Salaam, Irene Kiwia, Mwanzilishi na Rais wa TWA alisema kwamba jukwaa la Twaa
ni kama system ya GPS ambayo inasaidia kuwapa wasichana mwongozo wa
maisha. Jukwaa hili litasaidia kuwezesha
ukuaji wa ufahamu wa wasichana kwa kuboresha ujuzi wao, kuwawezesha kutekeleza
majukumu yao kwa kiwango cha juu na kuwasaidia kutambua uwezo wao kamili. Twaa
inaziba pengo lililopo ambapo wanawake wanataka kulipa fadhila kwa kuwanyanyua
wengine lakini wanakabiliwa na changamoto kwa kukosa muda kwaajili ya
mawasiliano ya ana kwa ana kutokana na kuwa na majukumu mengi katika jamii. Na
wasichana kote Afrika wanatafuta washauri wa kuwaongoza na kuwajenga lakini
wanakabiliwa na changamoto ya namna ya kuwapata.
Jukwaa hili linapeleka kazi za TWA nje ya mipaka ya Tanzania,
kwenda Afrika ambako taasisi hiyo inataka kupanua ushiriki wake.
"Nina furaha kuongoza ubunifu ambao
utaunganisha wanawake na watoto wa kike wa Afrika. Kwa fursa ambazo pia ndio
changamoto zinazokabili Afrika, nina imani kuwa suluhisho liko katika takwimu,
wingi wetu ndio silaha yetu. Kizazi kipya cha Afrika ni jibu katika kuziba
mwanya wa ukuaji wa maendeleo uliopo kwa sasa. Sio tu kwamba Africa ni bara
lenye idadi ya watu inayokuwa kwa kasi zaidi duniani, pia inakadiriwa kuwa
litakuwa ni bara lenye watu wenye umri mdogo zaidi duniani kufikia mwaka 2035.
Inakadiriwa kuwa Afrika itakaribia takribani nusu ya idadi ya watu ya dunia
nzima kufika miongo miwili ijayo. Sasa huu ndio mtaji mkubwa sana wa bara hili
na muda wa kukilea, kukiwezesha na kukiwekea misingi ya mahusiano kizazi cha
Afrika ni sasa". Alieleza zaidi Kiwia.
Bi. Sadaka Gandi, Mshauri maarufu, mwanasaikoloji na
Mwenyekiti wa TWA amesema ana lenga kuona wanawake viongozi katika Afrika
wanainua jukwaa hili kulipeleka mbele na kulitumia ipasavyo kuwapa ushauri
wasichana. "Twaa inawapa wanawake
suluhisho la uhakika na lenye ufanisi la kuwawezesha wasichana, kubadilisha
jamii na kubadilisha bara. Ni jukwaa linalowapa wanawake vinara nafasi ya
kuwekeza binafsi kwenye jamii kama
shukurani, kitu ambacho wanawake wengi wanakipenda. Tunatazamia kuwa jukwaa
hili litaanzisha utamaduni wa kujifunza miongoni mwa wasichana, na vile vile
kusaidiana. Kuna fursa nyingi sana nzuri ndani ya wanawake na wasichana wa
Afrika, tunatazamia kuona maisha ya wasichana yanaboresheka na kuleta athari
chanya Afrika zinazotokana na jamii ya wanawake waliowezeshwa.
Jukwaa hii ilianzishwa kwa ushirikiano na Shule Direct,
taasisi ya kijamii ambayo inatoa vifaa vya mafunzo kwa njia ya kidigitali kwa
wanafunzi Tanzania na Afrika nzima.
Inapatikana kwenye play store ya android katika kundi la application za
Lifestyle, na vilevile inapatikana kwenye mtandao kupitia www.twaa.co.tz.
Hii ni mara ya kwanza
ambapo Shule Direct imejiingiza katika ubia na taasisi nyingine kwa ajili ya
kupanua teknolojia yake katika kuwawezesha wanawake kuziba pengo la kusaidiana
ambapo ni muhimu katika maendeleo yao binafsi na ya kitaaluma. "Kama
taasisi inayoamini katika nguvu ya elimu kwenye kuibua vipaji, tunafuraha
kushirikiana na TWA katika kutengeneza jukwaa hili la kipekee linalosaidia
jinsi wanawake wanavyoungana, wanavyoshiriki na kujifunza. Nilivutiwa na kile ambacho TWA inatetea
ambacho ni kupanua fursa na kuhakikisha kujifunza kunakuwa ni sehemu muhimu ya
mafanikio ya wasichana. Wasichana
wanapaswa kushika hatamu, kumiliki fursa na kulitumia jukwaa
No comments: