By: Mohab Dominic
on 06:36
/
|
kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Simon Haule Akionyesha siraha ilikuwa inatumika na majambazi |
|
Haya ndiyo mabomu walikutwa nayo mabomu mawili ya kutupa kwa mkono |
|
eneo ambalo majambazi walikuwa maficho yao |
|
Kamanda simon Haule akiangalia moja ya korongo la maficho ya majambazi |
|
Risasi, mabomu. bunduki zilizotumika kwa uhalifu ambapo walikuwa wanakwenda kufanya shambulio |
|
Baadhi ya wananchi walifika chuma cha kuhifadhi maiti katika hospital ya mji wa kahama |
|
Wananchi wakiangalia miili ya majambazi walioletwa chumba cha kuhifadhi maiti kahama |
|
Moja ya siraha ilikuwa inatumika na majambazi |
|
Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga akichungulia moja ya korongo eneo la mwanva |
|
Moja ya ganda la risasi zilizotumika kwa kurushiana risasi |
|
eneo la tukio katika chuo cha mwanva mjini kahama |
|
eneo la mapambano na damu |
|
Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Simon Haule akiwa na mkuu wa upelezi wilaya kaham eneo la tukio ambapo majambazi watano waliuwa
WATU watano wanasadikiwa ni
majambazi walihusika katika mauwaji huko katika maeneo ya Kibiti Wilaya ya
Mkuranga Mkoani Pwani wameuwawa kwa kupigwa Risasi na Jeshi la Polisi Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga walipokuwa wakitaka kufanya jaribio la kuwapora
wafanyabiashara wa dhahabu .
Watu hao wameuwawa juzi katika
eneo la Mwanva katika kata ya Nyahanga Mjini hapa baada ya majibishano ya
Risasi baina yao na Polisi wa Doria waliokuwa zamu katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga Simon Haule alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
juzi katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo miili ya Majambazi
hayo imehifadhiwa ikisibiri kutambuliwa na ndugu zao.
Kamanda huyo alisema kuwa tukio
hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku baada ya jeshi hilo kitengo cha
intelejensi kupata taarifa ya kuwa kuna majambazi ambayo yalikuwa yamejipanga
kuvamia wafanyabiashara wenye maduka pamoja na wale wanajihusisha na ununuzi wa
madini ya Dhahabu.
Aidha Kamanda Haule alisema kuwa
baada ya polisi kupata taarifa hizo walienda katika eneo hilo ambalo lilikuwa
na vichaka pamoja na mapango ambayo yalisababishwa na uchimbaji holelea wa
mchanga na hivyo kuanza kurushiana Risasi kabla ya kuyazidi na kuyakamata
yakiwa yamejeruhiwa vibaya.
| |
Tag:
habari
matukio
MOHABMATUKIO.BLOGSPOT.COM's Admin
We are.., This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
No comments: