sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WALIMU KAHAMA MBIONI KUKIMBIA VITUO VYA KAZI.


Na Mohab Dominick
Kahama
Nov 11, 2013.
 

 MKURUNGEZI WA HALMASHAURI YA USHETU ISABELA CHILUMBA AKIWA OFISINI KWAKWE AKIJIBU SWALI ALILOULIZWA JUU YA TAFARANI  YA WALIMU WAKE KATIKA KATA YA MPUNZE SHULE YA MSINGI YA IPONYANHOLO NA WAANDISHI WA HABARI AMBAO AWAPO PICHANI 


WALIMUA wa Shule ya Msingi Iponyanholo kata ya sabasabini Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametishia kuikimbia shule hiyo kutokana na vitendo vinavyofanywa na Diwani wa kata hiyo Emanuel Makashi na Mtendaji wa kata hiyo Elias Mpigamanoni kwa vitendo  vya kuwalazimisha kuchangia shughuli za maendeleo katika kata hiyo kwa nguvu sambamba na kuwaweka mahabusu.

Wakiongea na waandishi wa habari wa nipashe katika kijiji cha mpunze Walimu hao walisema kuwa wamekuwa katika hali ngumu ya maisha kutokana na Mtendaji wa kata hiyo wakishirikiana na Diwani wake kuwalamisha kuchangia shughuli za maendeleo kiasi cha shilingi 28,500 na wengine walitoa kiasi shilingi 10,000   katika kata hiyo wakati wanakatwa kodi katika mishahara yao.

Walisema kuwa kwa sasa wamekuwa wakiishi maisha magumu shuleni hapo na wanapowaona viongozi hao wakiwa na migambo wakija katika shule hiyo walimu hao hulazimika kukimbia porini huku wanafunzi wakibaki wakiwacheka hali ambayo wanafunzi wamekuwa wakiwadharau.

Mmoja wa Walimu hao Almachius Chereales alisema kuwa  tarehe 22/10/2013 alitumiwa Migambo wawili waliokuwa na kamba na mawe mbele ya Wanafunzi na kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa katika Mahakama ya Mwanzo Mpunze iliyoamuru nikamatwe kwa kushindwa kutoa michango ya maendeleo ya kata.

Mwalimu huyo aliendelea kusema kuwa aliwekwa korokoroni kwa muda wa masaa 18 bila haya ya kupewa nafasi ya kujieleza hata kumuona Mtendaji wake wa kata Mpingamanoni aliyedaiwa kuwa na kufungwa kwa masaa hayo bila hata ya kupewa chakula kwa kipindi hicho.

Aidha Mwalimu huyo alisema kuwa Mtendaji huyo pamoja na Diwani wa Kata hiyo Makashi  wamekuwa wakifika katika shule hiyo na kusema kuwa hawatambui mchango wa watumishi hasahasa Walimu katika nchi hii na kuongeza kuwa mpaka Walimu hao wachange ndio watakapowaelewa.

“Sisi Kama Walimu na Watumishi wa Umma hatukupewa muda na Mwajiri wetu wa kuzalisha mali kwani mishahara tunayolipwa imebajetiwa kwa Walimu  na familia zetu kwa mwezi na kuniingilia hivyo ni kama kunidhalilisha”, Alisema Mwalimu Chereales.

“Mshahara wangu wa kila mwezi unakatwa kodi ( Income Tax) tofauti na Raia wa kawaida wasio wafanyakazi wa umma na pia bado kazi ninayoifanya ni ya umma na hivyo nimecgania maendeleo ya Nchi yangu kwa ujumla”, Aliongeza Mwalimu huyo.

Aidha aliendelea kutoa malalamiko kuwa alikamatwa mbele ya wanafunzi wake kama mtu aliyevunja sheria kubwa za nchi na kuongeza kuwa ili kushindwa kushiriki michango hiyo ni kuvunja sheria ipi?

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kahama Simoni Edwini aliptakiwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo alisema kuwa wao kama CWT wanafikiria juu ya kuifungulia  mashitaka Halmashauri ya Wilaya Kahama kwa vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa walimu katika kituo hicho.

“Haiwezekani Mwalimu akakimbizwa mbele ya Wanafunzi wake na kufungwa kamba kwa kosa la kutochangia maendeleo, leo mwalimu anweza akawa kituo hiki kesho kingine je kila kituo anachopangiwa atakiwa akichangia sehemu zote maendeleo”,Alisema katibu huyo wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kahama Simon Edwin.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya ushetu Isabela Chilumba alisema kuwa michango ya maendeleo kwa Walimu katika sehemu husika si lazima lakini unaweza kuchangia kama kuna uwezekano.

“Mbona sisi Wafanyakazi huwa tunachangia katika ujenzi wa sekondari na mambo mengine yaani hao walimu wameona nyinyi Waandishi wa habari ndio mnaweza kuwatatulia matatizo yao?, Alisema Isabela Chilumba Mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply