sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » SEREKALI IMESEMA HAITASITA KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO



Na  Mohab Dominick
Geita
Nov 11, 2013.
 

 RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MWENYE MIWANI NYEUSI KATI  WA KWANZA KUSHOTO NI MILIKI WA MGODI HUO EMMANUEL GUNGU NA WAKWANZA KULIA NI NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI STEPHEN MASELE NA MWISHO NI NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI MAJALIWA MAJALIWA AKIWA NA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA JANA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA KATIKA ZIARA YAKE YA SIKU YA PILI MKOANI HAPA.

SEREKALI  imesema kuwa haitaacha kuwasaidia Wachimbaji wadogowadogo katika mambo mbalimbali ikiwemo kuwapatia Leseni za Uchimbaji sambamba na maeneo ya kuchimbia ikiwa watafuata taratibu za kisheria katika kufanya shughuli hizo kihalali.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliyasema hayo wakati akifungua Mgodi mdogo wa Nsagali Gold Mine (NGM) unaomilikiwa na mwekezaji mzawa kutoka hapa nchini Emanuel Gungu katika mji wa Ushirombo juzi.

Rais Kikwete alisema kuwa Serikali haitaacha kumsaidia mchimbaji mdogo hasa  katika kumpatia mitambo mbalimbali kwa ajili kufanya shughuli hizo uchimbaji  hali ambyo itamfanya mchimbaji mdogo naye kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi.

Katika taarifa ya ujenzi wa Mgodi huo iliyosomwa na Mmoja wa wakurugenzi wake Njalu Silanga alisema kuwa Mgodi huo utanunua mchanga wa marudio kutoka kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuurudia kwa mara ya pili kitaalamu ili kupata mali iliyomo.

Silanga alisema kuwa kutokana na ujenzi wa Mgodi huo jumla ya watu 800 wamenufaika katika kupata ajira huku akiongeza kuwa watakuwa wakizalisha kiasi cha tani 120 za mawe zitakuwa zikisagwa kwa siku katika Mgodi huo.

Aidha aliendelea kusema kuwa Mgodi huo umegharimu kiasi cha dola za kimarekani  251 sawa na shilingi Bilioni 3.3 za kitanzania na kuongeza kuwa Kampuni yake mpaka kufikia hivi sasa tayari imekwishaanza kusadia mambo mablimbali katika sekta za Elimu, Maji na Afya katika aeneo la Katente mahali uliopo.

Hata hivyo Silanga alisema kuwa katika kuhakikisha Mgodi huo mpya unawanufaisha wakazi wa mji wa Ushirombo alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa umeme hali ambyo inafanya uzalishaji kuwa mdogo kwani wanatumia majenereta.

Katika ziara yake hiyo Mkoani Geita Rais Kikwete pia aliambatana na baadhi ya Mawaziri akiwemo Waziri wa ujenzi John Magufuli, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele, Naibu Waziro Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi Majaliwa Majali pamoja na maafisa mbalimbali wa Serikali.

mwisho





  

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply