Na Mohab
Dominick
Kahama
May 6, 2014.
HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA BAJETI ZA MICHEZO
CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga kimezitaka
Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kuwa zinatenga Bajeti za Michezo ambazo
zitawaendeleza vijana na kuwasadia kuachana na tabia ya kukaa vijiweni bila ya
kuwa na kazi ya za kufanya.
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Khamis Mgeja wakati akiongea na viongozi wa Chama cha Mapinduzi
kuanzia ngazi ya mashina na mabalozi katika Mji mdogo wa Isaka na kuangalia
ilani ya chama hicho kama inatelezwa.
Mgeja alisema kuwa Sekta ya Michezo ni kama kazi
kama ilivyo kwa kazi zingine za kimaendfeleo na kuongeza kuwa sekta hiyo ni
ajira na inawasaidia Vijana kwa kiwango kikubwa katika kupambana na ugumu wa
ajira hapa nchini.
“Tunaweza kukuza
ajira kwa kutumia michezo na sisi kama Chjama cha map[induzi Mkoa wa
Shinyanga tunaziomba Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa
zinaunga mkono na kusaidia vijana na katika sekta hiyo ya hichezo”, Alisema
Mgeja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Aidha Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa
Mkoa wa Shinyanga tumebahatika kupata Timu ya ligi kwa muda wa miaka 13 na kuongeza kuwa lazima tuiinge Mkono timu
yetu ya Stend United kwa sasa huku tukifanya jitihada za kuzipandisha timu
nyingine.
Kwa upande wake Mbuge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige
aliyeambatana na Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa jimbo lake limepania
kuboresha sekta ya michezo hali ambayo itakuwa ni kama ajira kwa Vijana wa
jimbo hilo.
Maige ambaye alitoa kiasi cha shilingi milioni 1.4
kwa Vijana wa Kata ya Isaka kama kuunga Mkono katika kata hiyo alisema kuwa kwa
sasa yupo katika mazungumzo na baadhi ya wafandhili kwa nia ya kuhakikisha kuwa
Jimbo la Msalala linakuwa na timu katika kiwango cha juu.
Wakati huhuo Mbunge wa Jimbo la Kishapu Selemani
nchambi alihaidi kuchagia jumla ya mipira 28 ambayo itatumika katika mashindano
ya Msalala cup ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni hali ambayo itakuwa ni
chachu kwa viongozi wengine kuchangia katika sekya hiyo.
mwisho
No comments: