sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KWENYE MIGODI

 mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akitoa maelekezo juu ya fursa tufanikiwe pamoja katika ukumbi wa hotel ya niteshi mjini kahama .
 msani wa sinema za bongo movie( bad boy )ibrahimu mbwana wakiwa na miliki wa blog ya Malunde kadama mwenye shati nyeusi katika ukumbi wa niteshi mjini kahama .
 msani marufu wasiti almasi akiwa na  mkurungezi wa  sanaa wa afrikani seven mosha kwenye semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya mgodi wa dhahabu wa buzwagi na african barrick gold mjini kahama .
 baadhi ya washiriki wa semina ya fursa  ya tufanikiwe pamoja wakiwa katika ukumbi wa nitesha.
 baadhi ya washiriki wa semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja na clouds fm na mgodi wa buzwagi african barrick gold mjini kahama  wakisikiliza maoni mbalimbali  kwa washiriki .
 baadhi ya wandaji wa sinema mjini  mwenye tisheti issa mbwana wakiwa  wakibadilisha  mawanzo katika senima ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya mgodi wa dhahabu wa buzwagi  na clouds fm mjini kahama .
 mwenye shati ya misitali mkono mirefu moja wa toa fursa toka clouds fm raymond mtani  akiwa na kikudi cha upendo sanaa cha mjini kahama wakibadilishana mwanzo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja .
 mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akitoa madaa juu ya kuwa na fursa ya tufanikiwe pamoja katika ukumbi wa niteshi hotel mjini kahama .
wasani marufu wa hapa nchini wasiti almasi na seven mosha wakisikiliza kwa makini muezeshaji hayupo pichani kwa fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya mgodi wa dhahabu wa buzwagi na clouds fm mjini kahama.
 afisa mahusiano wa mgodi wa dhahabu wa buzwagi wa african barrick gold dorothy bikurakule  wakibadilishana mawanzo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati wajasiliamali na clouds fm na mgodi huo .
 mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akitoa maelekezo kw kijana ambaye ni msani chipukizi katika ukumbi wa niteshe hotel kwenye semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja
 mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba alisimama akitoa fursa ya tufanikiwe pamoja katika ukumbi wa nitesh hotel mjini kahama .
 sikilizeni jamaani ndiyo maneno anayosema ruge mutahaba kwenye semina ya fusa ya tufanikiwe pamoja mjini kahama.
 baadhi ya wadau wa fursa tufanikiwe pamoja .
 mkurungezi wa clouds fm ruge mutahaba akisisitiza jambo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja /


 wasani katika pozi kwenye fursa ya tufanikiwe pamoja /
 majadiliano ya pamoja katika fusa ya tufanikiwe pamoja mjini kahama.
 majadiliano ya pamoja akitolewa na raymon mtani je ya ukumbi wa niteshi hotel .
 mazungumzo mwenye miwani ni msani seven mosha wakibadilisha mawanzo .
 badhi ya vikundi mbali mbali wakijadiliana
 majadiliano
 fursa ya tufanikiwe pamoja
 kaka hii ndiyo fursa tufanikiwe pamoja
 majadiliano ya pamoja.
 wadau wakisikiliza fursa ya tufanikiwe pamoja .
 mkuu wa wilaya kiomboi yahaya navada akiwa na muandishi wa gazeti la habarileo raymond mihayo kwenye semina ya fursa ya tufanikiwe pamoja .
  1.  wana habari wakiweka mambo sawa.
mjasilamali akisisitiza jambo juu ya fursa ya tufanikiwe pamoja kati ya clouds fm na mgodi wa dhahabu wa buzwagi african barrick gold katika ukumbi wa noteshi mjini kahama 


Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika mazingira wanayoishi ili kukabiliana na umaskini badala ya kulalamika kuwa hawana ajira wakati mwingine kujikuta wakishinda vijiweni.

Hayo yamesemwa jana na Meneja Mkuu mgodi wa dhahabu wa Buzwagi (ABG) Filbert Rweyemamu wakati was Semina ya fursa "Tufanikiwe pamoja"ulioandaliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Clouds Media Groups na kukutanisha makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wasanii,wajasiriamali,wakulima na wadau wa maendeleo Wilayani Kahama.

Semina hiyo ilikuwa  na  lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha wakazi wa Kahama wakiwemo wajasiliamali wadogowadogo kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao zizonaweza kuwapatia ama kunyanyua vipato vyao hususani katika maeneo ya Migodi.

Rweyemamu  alisema fursa inaanza pale mtu anapotambua kuwa kuna fursa katika mazingira yake hivyo  kuwaasa wakazi wa Kahama waangalie katika mazingira yao nini kinahitajika ambacho kinaweza kuwaingizia kipato ili kuondokana na umaskini katika jamii.

Alisema kuwa nchi jirani za Uganda na Kenya zimepiga hatua kimaendeleo kutokana na kwamba wananchi wake  wamechangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao ku hivyo kuwataka watanzania kujenga uthubutu kuleta mapinduzi badala ya kuendelea kulalamika kwamba ni maskini wakati watanzania wanazo akili za kuweza kufanya mambo makubwa.

“Asilimia kubwa ya watanzania ni vijana ,sisi African Barrick tumeungana na Clouds Media Group kukusanya vijana ili kuwaeleza kuhusu fursa hizo,tunaamini fursa inaanza hapo ulipo na tunawakaribisha kwenye migodi yetu,njooni tufanye biashara”,alisema Filbert Rweyemamu.

“Ndugu zangu mwenye macho haambiwi tazama,tunaacha mambo yanapita bila kuyafanyia kazi,tujenge uthubutu,tusiseme sisi ni maskini wakati tunayo akili ya kufanyia kazi mambo kadha wa kadha yaliyopo katika mazingira yetu”,alisisitiza Rweyemamu.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Iramba  mkoani Singida Yahaya Nawanda ,ambaye ana mradi wa ufugaji kuku katika wilaya yake alisema juhudi inahitajika pale mtu anapotaka mafanikio hivyo kuwataka wananchi kujituma katika kazi za mikono yao badala ya kukaa vijiweni kila wakati.

“Hakuna serikali ambayo itakuletea maendeleo vijiweni,unayesubiri serikali ikuletee pesa kijiweni kwako,utakaa hadi utachoka,tafuteni fursa katika maeneo yenu,undeni vikundi vya kuwaletea kipato,fanya kazi za mikono yako utapata pesa nyingi,mungu atakupa ridhiki kulingana na kazi zako",alisema Nawanda.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliwaeleza wakazi wa Kahama kuwa chochote kinachopatikana katika mazingira anayoishi binadamu ambacho kunaweza kumfanya mtu kuingiza kipato ni fursa inayopaswa kuchangamkiwa haraka.

Mutahaba aliongeza kuwa mji wa Kahama ambao unazungukwa na migodi ya dhahabu na sasa unaendelea kwa kasi unazo fursa nyingi lakini wananchi hawajajua kuzitumia hivyo kuwataka kuamka na  kuanza kutengeneza pesa ili kujiiunua kiuchumi.

Hata hivyo Mutahaba alisema ili kufikia malengo wananchi wanapaswa kujiamini na kutoamini kushindwa  huku akiongeza kuwa hakuna haja ya kutafuta kitu kipya kwani fursa ziko nyingi waangalie namna ya kuziboresha ili kujipatia kipato.

Mwisho



«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply