sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WAHUDUMU HOSPITALI KAHAMA WAKITHIRI KWA RUSHWA

mama huyu mkazi wa kata ya ushetu wilayani kahama akiwa muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wa kike hospitali ya wilaya ya kahama ilalamikiwa kwa kutoa huduma hafifu kwa kinamama wajawazito kwa huduma hiyo lazima kutoa kitu kindogo cha shilingi elf tano mpaka kumi .


Na  Mohab Dominick
Kahama
Agosti 11,2014
   
WAGONJWA  wanaolazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga hususuani katika wadi ya watoto wamekuwa wakijikuta wakipoteza maisha mara kwa mara kwa kinachodaiwa kuwa ni huduma mbovu zinazotolewa na Wahudumu wa Hospitali hiyoikiwa ni sambamba na kukithiri kwa Rushwa.

 Baadhi ya Wazazi wamekuwa wakilalamika kila siku kuhusu uongozi wa Hospitali hiyo bila ya tatizo hilo kufanyiwa kazi kwa kipindi muafaka hususani katika wadi ya watoto ambayo ndio yenye wagonjwa wengi hadi kufikia kulala kitanda kimoja wagonjwa wanne.


Wakizungumza na Mwandishi  wa Habari hizi aliyetembelea Hospitali hapo juzi, wagonjwa hao walisema kuwa kauli chafu,rushwa kwa baadhi ya manesi  ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kutokea kwa vifo vya watoto ambavyo visivyokuwa vya lazima hali ambayo inapaswa kukemewa mara moja ili kuondoa tatizo hilo.

Akizungumzia hali hiyo kwa masikitiko makubwa mmoja wa wagonjwa aliyelazwa na  mtoto wake katika wodi ya watoto Joyce Richard alisema kuwa pasipo kutoa chochote yaani fedha kwa wauguzi wa wadi hiyo  huwezi kupata huduma kwa wakati hali ambayo ilipelekea mtoto wake wa kwanza  kufaliki  dunia akiwa hospitalini humo wakati akipatiwa matibabu.

Aidha alisema kuwa kuwa kuna baadhi ya watoto katika wadi hiyo wempoteza maisha maisha huku wakiwa na uwezo wa kupata huduma bora hali ambayo alisema imekuwa ikiwakatisha tama hata katika kuwaleta watoto wao katika Wodi hiyo kutokana na huduma mbaya zilizopo katika wadi hiyo tena ya watoto.

“Mimi nililazwa na Mtoto wangu katika kitanda kimoja tukiwa wanne na mimeshuhudia zaidi ya watoto nne katika wodi hiyo wakipoteza maisha kwa uzembe wa wahudumu wa wodi hiyo hali ambayo inasikitisha kwa kweli, na kwa nini watoto wetu wapoteze maisha kizembe namna hiyo?”,Alihoji Joyce Richard


Alisema kuwa kiwango wanachotozwa na baadhi ya manesi hospitalini humo ni kuanzia shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa wale wenye uwezo na kuongeza kuwa  mtu anayetoa kiwango kikubwa cha pesa ndio anayeboreshewa huduma za matibabu na manesi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea mgonjwa husika mara kwa mara kujua hali yake.

Nae Magreth Peter alisema kuwa baadhi ya manesi wamekuwa na kauli za matusi , mara tu wanapohitajika katika kuangalia hali za wagonjwa hasa pale zinapokuwa zimebadilika na kuongeza kwamba inakuwa vigumu kwa mgonjwa kupewa kitanda wakati wa mapokezi hali ambyo inapelekea watoto hao kulala kitanda kimoja hadi kufikia wanne. 

Aidha kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo Joseph Fwoma alipoulizwa kuhusu malalamiko ya wagonjwa hao alikanusha nakudai kuwa wagonjwa wamekuwa hawafikishi malalamiko yao katika ofisi yake na kuongeza kuwa wamekuwa wakilalamika tuu nje ya ofisi.

Mwisho.






«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply