sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » Jamii nyahaswa kutobagua wanawake kuelekea usawa kijinsia

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo ya men engage meneja wa mradi huu emma mashobe mwenye miwani .
 waandishi wa habari wakimskiliza meneja wa mradi wa men  engage kwenye mafunzo ya vitendo yanafanyika mjini kahama mafunzo haya ni siku tatu .
 waandishi wa habari wa radio kaham fm mwenye shati ya blue bakari haridi  na mwenye gauni la  kitenge ni mwaandishi wa faraja fm gema wakisikiliza kwa makini emma mashobe wakati wa maswali na majibu juu ya usawa wa kijinsia .
 Mwaandishi wa ITV steven wanganyi akitoa maelezo juu ya mafunzo ya men engage .
 Meneja wa mradi wa men engage  emma mashobe akitoa somo la kuhamashisha wanaume na wavulana katika kuleta usawa wa kijisia kwa waandishi wa habari .
 Emma mashobe akionyesha jinsi hali hilivyo katika usawa wa kijinsia katika mafunzo ya vitendo kwa waanahabari .
Mwenye miwani meneja wa mradi wa men engage  Emma mashobe wakati wa majadiliano kwa waadishi wa habari.

Imeelezwa, mabadiliko ya kutoka maisha ya kuwabagua wanawake kuelekea usawa wa kijinsia  ni jukumu la jamii nzima na wala siyo la wanawake wenyewe na wanaharakati wa masuala ya jinsia peke yao.

Hayo yamebainishwa  mjini Kahama, kwenye semina ya waandishi wa habari wa shinyanga, semina iliyoandaliwa na shirika la care international Tanzania , linalotekeleza Mradi wa ushirikishwaji wa wavulana na wanaume katika kuleta usawa wa kijinsia (men engage).

Akifungua Semina hiyo ya siku tatu, meneja wa mradi huo Emma Mashobe amesema, kwa kipindi cha miaka miwili umeweza kuleta mabadiliko makubwa kwani jamii imeanza kuelewa umuhimu wa haki na usawa wa kijinsia.

Mashobe amesema, mradi umekuwa ukiwaelimisha wavulana mashuleni kupinga dhuluma kwa wasichana na kuhamasisha jamii kutambua mchango wao kwa familia na jamii kwa ujumla, na kwamba wanapaswa kupata stahiki zote ndani ya jamii.

Afisa ubora na mafunzo wa mradi David Magige amesema, kushirikishwa kwa wanaume na wavulana katika mradi kunatokana na ukweli kwamba mila na desturi za eneo hilo bado zinatambua mtoto wa kike kama chanzo cha uchumi kwa familia.
Amesisitiza, mabadiliko ya kweli yatawezekana tu iwapo wavulana na wanaume wataacha kuwaona wasichana kama sehemu ya burudani huku wakiwapa mimba na kuwaachisha masomo chanzo cha kuwepo kwa umaskini na ufukara kwa jamii.

Mradi wa Men Engage unatekelezwa kwa miaka mitatu wilayani Kahama huku ukihusisha kata za Bulyanhulu, Bugharama na Lunguya zilizoko katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Semina hiyo imehusisha waandishi wa habari 15 kutoka vyombo vya habari mbalimbali mkoani Shinyanga, kwa kuwa ndiyo vyombo vinavyoweza kufikisha haraka ujumbe kwa watu wengi na kwa mara moja.

 MWISHO



«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply