sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WANAFUNZI 302 WAKAA KWENYE MADAWATI 48

 Hii ndilo jengo la shule ya kadati kata ya isagehe wilayani kahama kama ilivyokutwa na waandishi wa habari .
 Hili  ndiyo Darasa la  shule ya wanafunzi 302 wakiwa chini bila ya madawati ya kusomea katika shule hiyo ya kadati wilayani kahama na mbuge wa huko ni mh  Ezekiel maige .
Hawa ni   baadhi ya wanafunzi wa kike katika shule ya kadati kata ya isagehe  wilayani kahama wakiwa katika mstari shuleni hapo .
 hivi ndivyo ilivyo baada ya kuanguka na upepo wa mvua serikali tuone huruma hawa walimu wetu.
 Hii ndiyo nyumba ya mwalimu kabla kuanguka.hivi ndiyo nyumba ya mwalimu kuu wanotoa vijana wetu kwenda vyuo vikuu vya tanzania.
 hili ndiyo Darasa la tatu katika shule ya kadati wilayani kahama kata ya isagehe mkoani shinyanga .
 Wanafunzi wakiwa darasani ndani shule yao tunatengemea kupata mawaziri hapa .



Na Mohab Dominck
Sept 14,2014
KAHAMA

 

Shule ya Msingi Kadati iliyopo Kata ya Jana tarafa ya Isagehe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madarasa hali inayosababisha baadhi ya wanafunzi kusomea nje chini ya mti na kusabaisha kusahaulika mara kwa mara.

Hayo yamesema na mwalimu mkuu wa shule hiyo Salu Luhendeka wakati akizungumza na gazeti la nipashe ambapo amesema shule hiyo ina jumla ya wanafuzi 302  kuanzia darasa la kwanza hadi la saba huku madarasa yakiwa matano na madawati 48.

Amesema kati ya madarasa hayo mawili yapo Katika hali mbaya zaidi ambapo hayana sakafu tangu yajengwe mwaka 1999, huku utoro wawanafunzi ikiwa ni changamoto kubwa kwani wazazi wamekuwa wakiwakataza watoto kwenda shule kwa lengo la kusaidia shughuli za Nyumbani.

Aidha ameioba  serikali kuzijali shule zilizopo pembezoni kwa kuhakikisha huduma zinawafikia walimu na wanafunzi na si kupendelea shule zilizopo katika maeneo ya karibu na mjini au sehemu ambapo miundombinu ya barabara na huduma zingine zinapatikana.

Mwalimu salu ametoa  wito kwa wazazi ambao pengine hawana mwamko wa kuwahamasisha wanafunzi kwenda shuleni.

Nao badhi ya walimu wa shule hiyo wametaja sababu zingine zinazochangia kuongezeka kwa utoro ni Nyakati za masika ambapo njia mbalimbali zinazoelekea shuleni hujaa maji na kulazimika shule hiyo kufungwa kwa muda ili kusubiri mito ikauke.

Mwalimu Salome Mwangosi ameiomba serikali kuwasaidia kuimarisha huduma za miundombinu shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kuimarisha barabara ili kuwasaidia kufuata huduma zingine katika kata jirani na sehemu zingine.

Kwa upande wake mwalimu Grace Urasa amesema uhaba   wa madarasa unasabaisha wanafunzi wanaosomea nje ya madarasa kushindwa kuelewa vizuri na kwamba wakati mwingine walimu wanashindwa kuwafundisha.

Hata hivyo amesema suala la ukosefu  wa barabara zinaunganisha kijiji hicho kimekuwa ni chanzo kikubwa cha kukwamisha ufanisi ya kazi zao huku wakihangaika kusafiri wakati wa masika kutokana na maji kutwama barabarani.

Shule ya Msingi Kadati ina jumla ya walimu 9 huku nyumba ya mwalimu ipo moja ambayo ni ya kudumu na zingine 8 ambazo si za kudumu zilijengwa na wananchi kwa lengo la walimu hao wanaishi  karibu na eneo la shule.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa shule  hiyo Michael Nkunga amekiri kuwepo kwa changamoto hizo licha ya uongozi wa bodi ya shule kuanza juhudi za kukabiliana na changamoto  hizo.

Nae mwanafunzi Agnes Charles ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo akizungumza na nipashe  akiwa nyumbani  amiomba serikali kuingilia kati suala la wazazi kuwakataza wanafunzi kwenda shule kwa lengo la kusaidia shughuli za nyumbani.

wanafunzi wa darasa la saba nchini wamehitimu masomo yao ya msingi ambapo  halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga  jumla ya wanafunzi 462 katika shule za serikali 72 na binafsi 8.

Mitihani hiyo ambayo ilianza jana  nan kumalizika wiki ilipita   katika mji wa kahama hali imeelezwa kuwa shwari na hakuna tukio lolote baya lililojitokeza katika kusimamia  mtihani huo.

Afisa elimu Msingi katika halmashauri ya Mji wa Kahama Aluko Aluko Amezungumza na hali  siyo kwa halmashauri ya mji wa kahama .

MWISHO








«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply