sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » SERIKALI YADAMIRIA KUWATAFUATIA WAFANYABIASHARA NG’OMBE MASOKO YA NJE

 Waziri wa mifungo na maendeleo uvuvi Titusi kamani mwenye miwani akiangalia shamba la kukuzia ngombe wilayani kahama mwenye shati jeupe ni mbunge wa kahama jemes lembeli .
 Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa kahama mwenye kuonyesha kidole lukasi makurumo akitoa tarifaa ya ukuzaji wa ngombe .
 mwenyekiti wa chama cha wanenepeshaji ngombe john nyenye akisalimia na mbunge wa jimbo la kahama mh jemes lembele  wa kwanza kushoto ni waziri wa mifungo na uvuvi Titus kamani ambapo ametembelea eneo la umoja wa nenepeshaji wa ngombe

 Baaadhi ya ngombe wakila chakula cha kunenepesha ngombe .
 Ngombe ambao wamepewa chakula wakingia katika zizi lao .
 Waziri wa mifungo Titus Kamani akisalimiana na baadhi wa viongozi wa unenepeshaji wa ngombe .
 Mh jemes lembeli akitoa maelezo kwa waziri   maendeleo  mifungo na uvuvi kuona jinsi ngombe wanavyonenepeshwa .


 Mwenyekiti wa wanenepashaji wa ngombe John nyenye akiongea na mbunge juu ya tatizo la soko la nje ya nchini .
 Waziri wa mifungo maendeleo na uvuvi Titusi kamani akiongea na baadhi ya wafungaji wa ngombe .

Waziri Titus kamani akukangua eneo la sehemu ya kunenepeshaji wa ngombe
 Moja wa wanenepeshaji wa ngombe Pamba Sesemuka .

 Waziri Titusi kamani mwenye miwani akiwa na wafungaji na wanenepeshaji wa ngombe .
Eneo la ngombe waziri Titus kamani akiangalia zizi la ngombe .


SERIKALI imesema kuwa ipo tayari kuwatafutia masoko ya Nje Wafanyabiashara wa ngombe hapa nchini iwapo watajiunga katika vikundi vya ushirika na kufanya biashara kwa kufuata sheria na taratibu.

Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya uvuvi Titus Kamani aliyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Ng’ombe Wilayani Kahama katika ziara yake ya siku moja Wilayani hapa.

Kamani alisema kuwa Wizara yake ipo tayari katika kuwasaidia Wafugaji wa Ng’ombe katika kuwatafutia masoko katika nchi mbalimbali ili waweze kufanya biashara ya ushindani zaidi kuliko ilivyo kwa sasa kwani wafanyabiashara hao wamekuwa watumwa na wale wa nje.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Busega aliwatahadharisha wafugaji hao kuacha kuuza ng’ombe wakiwa badi ni wazima kwani wanapoteza mali nyingi ikiwemo ngozi, Pembe pamoja na nyama hali ambayo inawanufaisha wale wafanyabiashara wa nje.

Awali katika taarifa yao  mbele Waziri Kamani Mwenyekiti wa chama cha wanenepeshaji Ng’ombe Wilayani Kahama John Nyenye alisema kuwa wanapata changamoto kubwa katika kufanya biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kukosa soko la Ndani la uhakika hususani katika migodi iliyopo Wilayani hapa.

Nyenye alisema kuwa wao kama wafanyabiashara wa Ngombe wanatumia muda wa siku 90 kwa kuwanenepesha ngombe hao huku wakiwanunua kwa bei ya kuanzia shilingi milioni moja katika Wilaya za Geita na Ngara huku wenyewe wakiwauza kati ya shilingi milioni moja na laki sita.

Nyenye alisema kuwa changamoto nyingine ni sehemu za malisho ya Ngo’mbe hao na upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo kunywa ambapo aliongeza kuwa mpaka kufikia hivi sasa bado Halmashauri ya mji haijawatengea maeneo ya malisho.

Aidha Nyenye alisema kuwa changamoto nyingine pia ni kutokuwa na majosho yakuwaogesha mifugo hapo pamoja na madawa hali ambayo inaweza kucgangia kuibuka kwa magonjwa kwa ngombe hao kwa kuwa wapo wengi katika shemu moja.

Katika ziara hiyo Waziri huyo alitembelea pia mabwawa ya samaki, Viwanda vya kucham bulia Pamba vya KCCL pamoja na kiwanda cha mafuta yua Pamba cha Kahama oil Mili vyote vya mjini Kahama.

Mwisho.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply