sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » ASKOFU MINDE WA JIMBO LA KAHAMA AHOFIA AMANI KUTOWEKA NCHINI

Baba askofu minde akitoa neno la kuimarisha amani nchini katika misa ya chrismas

 Baba askofu minde akiwapa watoto baraka za chrismas na mwaka mpya
watoto wakipokea baraka kwa mshika mkono baba askofu
pokea baraka za bwana ndiyo maneno ya baba askofu minde  kwa watoto 

njoo kwangu mpate baraka za bwana wetu 
 Baba askofu akisikiliza  neno la mungu
pokeni baraka za bwana wetu 

IMEELEZWA kuwa Amani Tanzania inataka kupotea Kutokana na watu kutomcha mungu na maadili kuporomoka kwa baadhi ya viongozi wa siasa nchini kutaka kujilimbikizia mali hasa kipindi cha uchaguzi unaoendelea hali ambayo inahatarisha Amani.

Hayo yamesemwa jana Mhashamu Askofu mkuu wa Jimbo katoliki la Kahama,Rudovick Joseph Minde katika maadhimisho ya siku ya Christmas katika mkesha wa misa Takatifu uliofanyika katika Parokia Tarajiwa ya roho mtakatifu Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Askofu alisema Watanzani tunahali mbaya Kutokana na amani inataka kupotea katika taifa hili ambapo inapotezwa na watu wachache wenye uchu na madaraka ambao wanalengo la kujilimbikizia mali zisizokuwa na tija yoyote hasa kipindi hiki cha mpasuko wa kisiasa.

Hata hivyo Askofu Minde amekemea watu wanaoifanya sikukuu kuwa nidiyo siku ya nafasi ya kufanyia maovu kuvuruga amani ama ndiyo sehemu ya mapambo,kula vizuri,kutembea barabarani bali aliwaeleza kuwa maana ya Christimas ni tendo la upendo wa juu mungu kumpenda mwanadamu.

Amewataka waamini wa madhebu ya kikristo kuiombea Amani ya Tanzania kwa kufanya ibada makanisani na kusema kuwa amani ikipotea hakuna mtu atakayeweza kuirudisha na kusema kuwa ili kuondoa changamoto za kimaisha ni lazima wafanye yale yampendezayo mungu nakuongeza amani ya familia ni kusali pamoja nakushirikishana mambo mengi.

Amesema kuwa maadhimisho haya hufanyika kila mwaka ambapo wakristo wengi ulimwenguni huungana kwa pamoja kusherehekea siku hiyo muhimu kwa lengo moja la kuendelea kumshukuru mwenyezi mungu
 Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply