sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WAZIRI MKUU AZUNGUMZIA UCHAGUZI MKUU 2015


Waziri Mkuu Mizengo Pinda (mwenye tai) akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea maabara ya kisasa ya sayansi ya Chuo Kikuu cha Mkwawa (MUCE) Iringa, katika ziara yake ya siku tano ya kutembelea miradi ya maendeleo mkoani Iringa.

AKIWA katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku tano mkoani Iringa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewaonya viongozi na chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuwachaguliwa wananchi viongozi.

Aliyasema hayo kwa nyakati tofauti juzi, katika ziara aliyofanya katika vijiji vya Mlowa, Magozi na Kiwele, wilayani Iringa, kutembelea shughuli za maendeleo.

“Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Hili ni zoezi muhimu sana kwa nchi ya kidemokrasia kama hii. Tuwaache wana CCM na wananchi waamue wenyewe, wasisirutishwe kuchagua viongozi wasiowataka,” alisema.

Alisema wagombea hao ni kwa nafasi zote zitakazoshindaniwa katika uchaguzi huo ikiwemo ya udiwani, ubunge na rais.

Alisema CCM ikifanya makosa ya kuwapatia wananchi wagombea wasiowataka itaruhusu wagombea wazuri kukimbilia upinzani na kujiweka katika hatari ya kuangushwa katika uchaguzi huo.

“Tuwaunge mkono wagombea wanaokubalika, wenye sifa ya kutuletea maendeleo. Tukifanya makosa tutaanguka asubuhi tena anguko la mweleka,” alisema.

Alisema pamoja na kuwapa wana CCM uhuru wa kuchagua, watajiangusha kama watawachagua kwasababu ya rushwa au ofa mbalimbali zikiwemo bia.

Akizungumzia umuhimu wa uchaguzi huo kwa CCM, Pinda aliwataka watanzania kwa ujumla wao kujiandikisha katika daftarai la wapiga kura ili wawe na uhalali wa kuchagua viongozi wanaowataka wakati ukifika.

“Tupo katika hatua za mwisho za kuanza uandikishaji kwa kutumia teknolojia mpya ya BVR na mimi mwenye nitafanya uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Njombe,” alisema.

Waziri Mkuu alisisitiza kila mwenye umri wa kupiga kura (kuanzia miaka 18 na kuendelea) asiipuuze nafasi hiyo kwani mbali na kadi ya mpiga kura kupiga kura lakini pia itatumika kama kitambulisho wakati mchakato wa kutoa vitambulisho vya utaifa ukiendelea.

Kuhusu  Katiba Mpya, Waziri Mkuu aliwataka watanzania kutumia uhuru wao kujitokeza kwa wingi kupigia kura ya ndio au hapana katiba hiyo inayopendekezwa.

“Jitokezeni kwa wingi mkaipigie kura. Kazi iliyofanywa na bunge maalumu la katiba ilifanywa kwa umakini mkubwa, ni katiba inayojali makundi yote katika jamii, msiwasikilize wanaotaka msusie,” alisema.

Alisema kabla ya zoezi hilo serikali itakahakikisha inasambaza nakala ya katiba hiyo ili watanzania popote walipo waweze kuipitia ili wajiridhishe juu ya maeneo yanayopotoshwa.

“Kwahiyo tutsambaza katika kata zote, vijiji, mitaa, makundi ya kijamii na taasisi mbalimbali zikiwemo za dini,” alisema.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameipongeza CCM Mkoa wa Iringa kwa kuongoza kitaifa katika Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba mwaka jana.

“Kwa CCM, mkoa wa Iringa umeongoza kitaifa kwa kujipatia ushindi wa asilimia 98. Ni asilimia mbili tu ndio tuliwaachia wapinzani na sehemu yake zimeto pale mjini Iringa na tunajua ni kwasababu gani,” alisema.

Alisema ushindi huo ni kiashiria tosha kwamba katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais mkoa wa Iringa utafanya vizuri kama ilivyofanya katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa.
Mwisho 



 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply