sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » KATIBU WA ITIKADI UENEZI NA KATIBU WA UCHUMI FEDHA WILAYA YA KAHAMA ATIMUKIA CHADEMA

                                          ISAYA BUKAKIYE SIMON



 KAHAMA

SIKU chache baada ya kutangazwa kwa kura za maoni ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya kahama mkoani shinyanga baadhi ya wanachama hicho katika kata ya kahama mjini wame kihama chama na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Akiongea blog hii   mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema  wilaya Juma Protasi alisema kuwa jana wanachama zaidi ya 50 wamejiunga na chama chake akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ushetu Isaya Bukakiye pia ni mweka hazina wa wilaya ya kahama  ambae ni miongoni mwa waliokabidhiwa  kadi za chama.

Alisema kuwa miongoni mwa waliorudisha kadi za chama cha mapinduzi ni pamoja na mabalozi 12 kutoka kahama mjini,mwenyekiti wa CCM tawi la Majengo na wafuasi wengine wanaendelea kujiunga na kutokana na mizengwe iliyotumika katika uchaguzi wa kura za maoni.

“Tumepokea mabalozi 12 na mwenyekiti wa ccm tawi la majengo kutokana na wao kutoku tendewa haki katika kura za maoni hasa wakati wa kumpisha mgombea ambao wao walikuwa wakimhitaji,ambapo walikuwa wakipiga kura walikuta majina yao yameuzwa kwa watu wengine na kwajambo hilo ndilo limepelekea wao kujiunga na Chadema” alisema Protasi.

Katikia hatua nyingine alisema kuwa chama cham Chadema kinaendelea kuimalisha ngome zake na kuandaa mazingira ya ushindi ndani ya majimbo yote matatu ambayo ni pamoja na Ushetu,Kahama mjini pamoja na Msalala lakini pia ikiwa ni pamoja na kupokea wananchama wapya wanaohama kutoka katika vyama vingine vya siasa.
Mwisho.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply