sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » SERIKALI WILAYANI KAHAMA YAKIRI MAJI YA MGODI WA BULYANHULU YALIKUWA NA SUMU

 Baadhi ya wanakijiji cha namba 9 kakola wakiwa katika mti wao mkubwa kwa ajili ya kutoa kero zao kwa waana habari kwa kuchelewa kulipwa kwa fidia yao ambapo zaidi ya kaya 138ambazo zimeasidhilika na maji hayo ya sumu.
 Mmoja ya wanakijiji cha namba tisa akiongea na blog hii juu ya tukio hilo la maji ya sumu kuingia katika mashamba yao na kuzuiwa kulima kitu chochote katika eneo hilo la namba tisa .
 Mkazi wa kijiji cha namba tisa kakola akiongea juu ya kulipwa kwa fidia ya mashamba yao na baadhi yao walipoteza mifungo yao .

 Peter mayunga akitolea ufafanuzi jinsi maji  nyenye sumu kutoka katika mgodi wa Blyanhulu Acacia .

 
Baadhi ya wanakijiji wakitoa malalamiko yao mbele ya vyombo vya habari
 

 Mmoja ya kisima cha kijiji cha namba tisa ambacho kilikuwa na sumu ya kuchaka chua Dhahabu,  Ambacho migodi wa Blyanhulu ilikifunga ili wananchi wa kijiji hicho wasiwenze kuchota maji hayo.kama jinsi kinavyoneka kufungwa kwa kisima hicho kwa Ngufuli kubwa .
 Moja ya Tuta kubwa ambalo lipasuka  kwa  maji ya mvua kunyesha kubwa na kupasuka na kuwanga maji hayo nje ya mashamba ya wakazi wa kijiji hicho na kulete madhara  makubwa.

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiangali bwabwa kubwa maji kwa ajili ya kunyeshea mifungo yao ambapo sumu hiyo ilimwangikia humo .
 Watoto wa vijiji vya namba Tisa wakiwa wakicheze kwenye maji nyenye sumu kutoka mgodi wa Bulyanhulu ,kakola ambapo maji hayo yana sumu.
 Miti ya eneo hilo nayo ilikaauka na majani pia yalikauka .

 Eneo la Bwawa la kunyeshia mifungo ya wanakijiji cha namba tisa ambapo awali walikuwa wanakunywa maji katika bwawa hilo .
 Mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akiongea na vyombo vya habari juu ya malipo ya fidia kwa wananchi wa kijiji cha namba tisa kakola.
 Mkuu wa wilaya akisoma moja ya yaraka za Nemc.juu ya majibu ya kulipwa fidia kwa wakazi wa eneo hilo lenye kaya 138 ambao wameadhilika kwa maji hayo ya sumu .
Mmoja ya Gati la maji lilotengwa na mgodi wa Blyanhulu kwa ajili ya wakazi wa kijiji hicho vcha namba tisa ambapo wakazi wa eneo hilo wanapata huduma ya maji salama .

SERIKALI kupitia Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) imesema kuwa maji yaliotiririka kutoka katika moja ya  Mabwawa ya maji ya Sumu katika Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu na kuingia katika kijiji cha Namba tisa katika kata ya Kokala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga mapema mwezi januari mwaka huu yalikuwa na sumu.

Akiongea kwa niaba ya NEMC Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema kuwa baada ya maji hayo kupasua moja ya Mabwawa yanayofidhi sumu kali aina ya synide hiyo kuingia katika kijiji hicho yalisababisha uharibifu mkubwa ikiwemo mazai, vyanzo vya maji pamoja na mifugo.

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo Serikali ya Wilaya ya Kahama kupitia Mkuu huyo wa wilaya ilisitisha shughuli za Kilimo pamoja kuzua Wananchi wa Kijiji hicho kutumia maji ya Visima hadi hapo Baraza la hifadhi ya mazingira nchini litakapoto majibu baada ya kufanya uchunguzi.

Aliendelea kusema kusema kuwa baada ya NEMC kufanya uchunguzi waligundua kuwa sumu iliymwagika katika Kijiji hicho ilikuwa na kiwango cha 1.126 PPM kiwango ambacho ni kikubwa na kuitaka Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi huo wa Bulyanhulu kuhakikisha kuwa inawafidia Wananchi wa Maeneo ili wakanunue chakula baada ya kukaa muda miezi nane bila ya kujishughulisha na Kilimo.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa kiwango cha  sumu cha kawaida kinatakiwa kuwa 0.001PPM na kuongeza kuwa kutokana na NEMC kugundua kuwa maji yale yalikuwa na sumu ni bara sasa Kaampuni hiyo ya Madini ikawaadia Wanachi maeneo ili waweze kufanya shughuli za uchimbaji kwa kuwa eneo hilo lipo ndani ya leseni yao.

Hata hivyo alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya udhibiti wa Hifadhi ya Mzingira  ya namba 191 kifungu cha 197 kipengele cha namba moja hadi namba nne  inasema kuwa kitendo kichofanywa na Kampuni hiyo cha kutiririsha maji ya sumu katika makazi ya Wananchi ni kosa.

Kwa upande wa Wananchi wa Kijiji cha namba tisa kata ya Kakola wakiongea na Waandishi wa Habari walisema kutoka na sumu hiyo kuingia katika mashamba wameiomba Serikali kuhakikisha kuwa wanalipwa fidia zao kwani kwaa kipindi kirefu wamekaa bila ya kufanya shughuli zozote za kimaendeleo hali iliyowaaathiri kiuchumi.

Mmoja wa Wanachi hao Mayunga  Peter alitoa lawama zake kwa Mgodi huo kwa kushindwa kuwapa huduma kwa kipindi chote cha miezi nane ingawa eneo hilo la Kijiji lipo ndani ya Leseni ya Mwekezaji na kuongeza kuwa kwa kuna baadhi ya Wananchi wamekuwa wakisumbuliwa na Magonjwa kama ya kuumwa kichwa pamoja na Miguu kutokana na kuathirika na Kemikali hiyo.

Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply