sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WANAOHUJUMU CCM,YUMO GASPER, NI WALE WA MCHANA CCM, USIKU UKAWA

 

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.







Akiwahutubia wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Dk. Magufuli aliwataja hadharani baadhi ya makada hao ambao wamekuwa wakiipigia kampeni CCM mchana na usiku wakiwapigia wapinzani.
“Kuna baadhi ya wana-CCM wanatujuhumu sana, wengine nawajua hata majina yao bahati nzuri huwa sisemi uongo bali ukweli, kuna huyu Gasper mchana tunakuwa naye CCM lakini usiku anaungana na wapinzani,” alisema.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Dk. Magufuli ilipokelewa kwa mshangao na baadhi ya wananchi na wanachama waliokusanyika uwanjani hapo, kwa kuwa baadhi ya makada hao walikuwa wameketi jukwaa kuu wakifuatilia hotuba yake.
Waandishi wa habari hizi walimshuhudia meneja kampeni wa mgombea huyo, Abdallah Bulembo, akimfuata Magufuli na kumnong’oneza ,ghafla Magufuli alibadilisha na kudai msaliti ni Gasper Anthony wala si Gasper Kileo aliyetajwa awali.
Hata hivyo, Magufuli baada ya kumaliza hotuba yake alimfuata kada wa CCM mkoani Shinyanga anayetumia jina la Gasper  aliyeonekana kupaniki na kumkumbatia huku akimtuliza na kuendelea na msafara wake.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply