sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » LIPUMBA MAALIM SEIF WAKUTANA WAONGEA MAMBO MAZITO

 



Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ZEC kutangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar October 28 2015, Kiongozi wa zamani wa chama cha CUF, Professor Ibrahim Haruna Lipumba na mgombea Urais wa Zanzibar kwa mwamvuli wa CUF na Umoja wa vyama vya UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad wamezungumzia kuhusu kuchukuliwa kwa hatua hiyo.


“Nimeshtushwa na hatua hiyo hasa ukizingatia Uchaguzi umefanyika tarehe 25 leo ni tarehe 28, na sababu ambazo Mwenyekiti amezitoa ni mambo ambayo yangeweza kujulikana mapema sana… Tume ya Uchaguzi ya Taifa ambayo inatangaza matokeo ua Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa inatangaza Kura za matokeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ambazo zimefanyika kwenye uchaguzi huohuo mmoja na Tume haijasema kwamba uchaguzi ule ulikuwa mbovu.”- Professor Ibrahim Haruna Lipumba.



“Hata watazamaji wa Kimataifa wamesema utaratibu wa kupiga Kura na kuhesabu vituoni ulikwenda vizuri… nashukuru viongozi wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewaomba Wazanzibar kuwa watulivu wakati suala hili linashughulikiwa.” >>> Prof. Lipumba.



“Ilipaswa iundwe Tume ya Majaji watazame tamko alilolitoa lina uhalali gani, wazungumze pia na Wajumbe wa Tume ya uchaguzi kwa sababu tamko hilo limevunja Sheria halina uhalali wa kisheria.”

Hili ndio jibu la Professor Lipumba kuhusu anayeweza kumaliza tatizo lililotokea Zanzibar >>> “Mtu ambaye ana uwezo na wajibu mkubwa kwenye hili ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu yeye ni Rais na Mwenyekiti wa CCM, ashauriane na Rais wa Zanzibar ili akubali kuunda Serikali ya kitaifa, imefika wakati Dk. Shein aoneshe ukomavu wa kisiasa.”



Kuna watu wamelalamika, nimemsikia Edward Lowassa amelalamikia matokeo ya Uchaguzi, haya ambayo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ameyaeleza yanaongeza nguvu kwa Mheshimiwa Lowassa kwamba hata Tanzania bara mambo hayakwenda sawa… Hatua aliyochukua Mwenyekiti imevunja Sheria, isipotokea ufumbuzi mapema, patatokea vurugu.” >>> Professor Ibrahim Haruna Lipumba.

HAPA NAANZA NA KILE ALICHOKISEMA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.

“Chama cha CUF kimepata taarifa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ametangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu bila kuwashirikisha Makamishna wenzake wa Tume ya Uchaguzi…. CUF imeshtushwa na taarifa hii ambayo iko kuinyume na Sheria za uchaguzi ya Zanzibar, Mwenyekiti hana mamlaka ya kufuta Uchaguzi huo.” >>> Maalim Seif Sharif Hamad.



“Mwenyekiti hakutafakari kwamba kuufuta uchaguzi Zanzibar kunaathiri pia Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu wapiga Kura ni walewale waliomo kwenye daftari la wapiga Kura wa ZEC.” >>



“Rais wa Jamhuri ya Muungano hawezi kupatikana kwa kupigiwa Kura na wananchi wa Tanzania bara pekeyake… Tunatambua kwamba hatua hii imekuja baada ya majaribio ya kulazimisha ushindi kushindikana.



“CUF hatutambui uamuzi huo wa Mwenyekiti wa Tume ya ZEC, tunaitaka Serikali na CCM kuiacha Tume iendelee na uhakiki wa matokeo na itangaze mshindi… Tunatoa wito na kuomba Wazanzibar kwa ujumla kubaki watulivu..” >>> Seif Sharif Hamad.

Sauti yote ya Maalim Seif Sharif Hamad hii hapa kama umepitwa na hii taarifa,pia kuna sauti ya Professor Ibrahim Lipumba

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply