sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MAAJABU YAIBUKA SHINYANGA

Duh!! Maajabu Shinyanga!! WATU WAWILI WAMEFARIKI KWA SHOTI YA UMEME KWENYE NYUMBA ISIYO NA UMEME...USHIRIKINA WATAJWAMiili ya marehemu Marco Martine(29) kushoto na Paskaline Nikomedi(26) baada ya kupigwa na shoti ya umeme katika nyumba ya mzee Zabron Mazoya ambayo haina huduma ya umeme katika mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo maarufu kwa jina la Upongoji mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo Mohammed Hizza Saguti akielezea jinsi tukio lilivyotokea
Mwenyekiti wa mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo Mohammed Hizza Saguti akionesha sehemu ambayo ulikuwa umefungwa waya kwa ajili ya kuanikia nguo,ambao unadaiwa kusababisha vifo vya watu wawili

Kushioto ni Diwani wa kata ya Masekelo Samwel Sambayi akizungumzia tukio hilo ambapo amewataka wananchi kusubiri uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha vifo hivyo badala ya kukimbilia kuamini kuwa ni imani za kishirikina.

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Kushoto ni bwana Paul Maduhu jirani aliyekuwa wa pili kufika eneo la tukioa, aliyenusurika kifo katika tukio hilo akionesha mahali palipotokea tukio hilo na kueleza kuwa baada ya kufika katika nyumba hiyo alikuta watu hao wameanguka chini huku waya uliokuwa unatumiwa kuanikia nguo ukitoa cheche za moto huku miili ya marehemu ikitoa moshi. 
Mwenyekiti wa mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo Mohammed Hizza Saguti akionesha waya wa Cable(TV) ambao unadhaniwa kuwa huenda ndiyo umesababisha shoti hiyo,uliopita nyuma ya nyumba ya mzee Zabron Mazoya kuelekea nyumba ya jirani 

Mwenyekiti wa mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo Mohammed Hizza Saguti akionesha nyaya za cable ambazo huenda ndiyo sababu ya shoti ya umeme Nyuma ya nyumba ya mzee Zabron Mazoya,kushoto ni nyumba ya jirani yake,ambayo ina umeme,ambapo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema huenda kuna watu walikuwa wanatumia umeme kwa njia ya wiziNyumba za mzee Zabron Mazoya,juu ni nyaya za cable ya Tv zinadaiwa kuwa huenda ni chanzo cha shoti hiyoWaya wa Cable ukiwa juu ya nyaya za umeme wa TANESCO ambazo zinadaiwa kuwa chanzo cha shoti ya umeme katika nyumba ya mzee Zabron Mazoya


Wananchi wakionesha waya mwingine wa kuanikia nguo katika nyumba hiyo
Mzee Zabron Mazoya mgonjwa wa mguu wa kushoto ,mmiliki wa nyumba akionesha taa/tochi anayotumia wakati wa usiku kwani nyumba zake zote hazina huduma ya umeme.Nyumba ya kubwa ya mzee Zabron Mazoya,nyuma yake ni nyumba zake zingine ambapo alikuwa na mpangaji mmoja pekee Paskaline aliyefariki kwa kile alichodai katika mazingira ya kutatanishaKulia ni Mzee Zabron Mazoya akielezea juu ya tukio hilo

Kumetokea tukio la aina yake leo saa moja asubuhi mjini Shinyanga,ambapo kwatu wawili wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa kile kinachotajwa kuwa ni shoti ya umeme kwenye nyumba isiyokuwa ya umeme mali ya mzee Zabron Mazoya iliyopo mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo maarufu Upongoji katika manispaa ya Shinyanga.-kwa hisani ya  Kadama Malunde-Malund.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply