Mkuu wa wilaya ya kahama DC Fadhili Nkulu Akiongea na waandishi juu ya uhamuzi wake wa kuweka rumande Mtendaji wa kata na Afisa Afya wa Mji
KAHAMA
MKUU wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu amewaweka mbaroni
Maafisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kosa la kuacha uchafu
ulikokuwa katika Barabara kuu ya Mji wa Kahama ya kwenda katika Nchini za jirani za Rwanda na
Burundi hali ambayo imesababisha eneo hilo kuwa mrundikano mkubwa wa taka zilizokuwa zikitoa harufu mbaya.
Maafisa Afya hao waliowekwandani na Mkuu huyo wa Wilaya ni Johanes
Mwebesya na mtendaji wa kata ya
nyasumbi Enocent kapeli kwa kosa la kutoa uchafu hulioko
mwanzo wa barabara kuu ya kuingia katika mji wa kahama eneo la Phatom na kuacha wanachi wakitupa taka katika eneo hilo
ambalo halistahili.
Tukio hilo limetokea jana wakati Mkuu wa Wilaya ya Kahama
Fadhili Nkulu akipita eneo la phatom akielekea halmashauri ya ushetu kwa ajili ya
ziara ya kikazi za kawaida na kuona lundo la uchafu katika barabara hiyo kuu ya kuingia Kahama Mjini jambo ambalo linalita
sura mbaya kwa mji wa Kahama.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya Fadhili Nkulu alisema alitoa maagizo kabla ya kuondoka
kwenda Halmashauri ya Ushetu mbele ya Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba pamoja na Mtendaji
wa kata hiyo na afisa afya wa kata hiyo kuwa akirudi kutoka Ushetu akute uchafu huo umeondolewa hapo haraka sana jambo
ambalo halikutekelezeka.
Nina waambia nyinyi maafisa Afya
nikirudi toka ushetu jioni nikute lundo hilo la chafu limeondoka
eneo hilo na pawe safi sitaki kuona takataka katika eneo hilo kwani hapo ni
katika sura ya Wilaya ya Wilaya hata mgeni akija katika Mji wa Kahama cha
kwanza kuona ni uchafu uliopo eneo hilo”, Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama
Fadhili Nkulu.
“Watumishi hawa wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Wamezoea kufanya kazi
kwa mazoea jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi haiwezekani mwanzo tuu wa
kuingia Mjini wa Kahama kunakutana
na Dapo la uchafu je huko ndani kutakuwa
na hali gani kama mwanzo tu kunakuwa na Mrundikano wa taka kiasi hicho.”Alisisitiza
Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo alisema kuwa wito wake kwa sasa kwa watumishi wa umma ni
kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea na kuakikisha kila moja wetu anatunza
maeneo yake ya kazi na kufanya usafi katika maeneo yaliomadhubuti kwa hali
ambayo itachangia kiasi kikubwa kuuweka Mji wa Kahama katika hali ya usafi hali
ambayo inaweza kuchangia katika kuzuia magonjwa ya milipuko kama pikindupindu .
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu pia aliwataka
Watumishi wa Serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani Serikali hii ya
awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli na kauli yake ya hapa kazi
inatakiwa kila mtumishi ajitume katika kufanya kazi za kuwahudumia Wananchi
hali ambayo italeta mabadiliko makubwa katika utendaji wa kazi.
Mwisho
|
No comments: