Moja ya mteja wake ambaye jina lake alikuweza kufamika mara moja ,akipongeza kwa kufanya biasha yake kuonekana katika ubora kama mjasiliamali mdogo
DODOMA Kijana Moja mjasilimali mkazi wa mji wa Dodoma Willfrend
makundi miaka (25) ambaye ni
mfanyabiasha ya matunda katika mtaa wa mtendeni mji hapa amefanikiwa kwa kuuza
matunda kwa mtaji wa shilingi elfu kumi na mbili kama mtaji wake na kununua gari
kwa ajili ya kuuza matunda katika mji wa Dodoma.
Akiongea kwa uchungu mkubwa na mohabmatukio.blogspot.mji
Dodoma alisema yenye aliaza biashara yake ya kuuza matunda katika kipindi zaidi
ya miaka kumi mjini hapa kwa mtaji wa kiasi cha shilingi elfu kumi na mbili.
Changamoto hakuna siku ambayo siwezi kusahau ambapo nilikopa
fedha kwa jamaa zangu kwa ajili ya kununua matunda wakati huo mimi nilikuwa
naunza kwa toroli la kusukuma,matunda yangu yote yalikamatwa na manispaa
yakaalibika zaidi ya laki tano nilipoteza.
Sikukataa taama nikarudi upya na biashara yangu hapo sasa
nikaza mkanda kweli kweli basi
niliendelea na biashara yangu na wateja wangu walikuwa wamekwisha nizoe sana
kwa sababu nilikuwa karibu na hotel moja hapa mtaa wa mtendeni Dodoma jamaa
zangu tena na juhudi zangu nikanza tena biashara ya matunda.
Hivi sasa mimi ni mtaji wa zaidi ya milioni 4 na nikafikiria bora ninunue gari ndogo kwa ajili yah ii biashara
na niwenze kuwepuka na matatizo ya mara kwa mara na manispaa ya Dodoma kwa
utunzaji wa mazingira na usafi na ubora wa matunda yangu kwa wateja wangu
wadodo na wanapita hapa.
Mafanikio mpaka sasa ni vijana wanne ambao ni wasaindizi wangu katika biashara hii yangu kwa sababu wapo wengine wanatoka katika ofisi za bunge kuja kula hapa matunda na hapa karibu na ofisi za makao makuu CDA kwa ajili ya matunda.
|