sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MWANAMKE KAHAMA AFUNGWA JELA MIAKA KUMI AKAMATWA NA MABOMU PINGU, VISU VYA KIJESHI

Moja ya Bomu la kutupwa kwa mkono aliokamatwa nayo Aisha juma mkazi wa kata ya  nyahanga wilayani kahama 



 Pingu ambazo alikamatwa nazo  Aisha  juma 

Risasi alizokamatwa nazo Aisha juma mkazi wa kata ya nyahanga wilayani kahama pamoja na mabomu ya kutupa kwa mkono

KAHAMA 
Mahakama wilaya ya kahama mkoani shinyanga imehukumu kifungo cha miaka 10  Aisha Juma kwa kosa la kuutwa na hatia ya kukamatwa na siraha mabomu ya kutupa na mkono pamoja  visu na pingu  katika kata ya  nyahanga. 

Akiongea mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo  Vodia Kiharuzi mwendesha mashitaka Athumani kisango aliambia mahakama hiyo kuwa Aisha juma alikamatwa maeneo ya nyahanga majira ya joni akiwa na silaha hizo.

Aidha mwendesha mashitaka aliambia mahakama aisha alikamatwa tarehe 11 mwezi wa kumi nyumbani kwake akiwa na silaha hizo,kwa mujibu wa sheria cha 21 cha mwaka 2015 ni kosa kukutwa na risasi.

 Akitoa  hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,Evodia Kyaruzi alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ameridhika kuwa, mshitakiwa  walikutwa na mabomu hayo ya kinyume cha sheria na kumtia hatiani kwenda jela mika kumi .

Hakimu huyo alisema kuwa,mahakama hiyo baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote imeridhika nao, hivyo washitakiwa wanatiwa hatiani kwa kifungo cha adhabu ya sheria cha 21 cha mwaka 2015.

  Awali katika ushahidi wake Mwendesha mashitaka wa polisi upande wa Jamhuri,  Athumani kisango na upande wa mashahidi uliotolewa  mahakamani hapo waliiambia mahakama hiyo kuwa,mshitakiwa  walikutwa na mabomu hayo  katika eneo la nyahanga  .

Kwa upande wake  mshitakiwa   katika utetezi wake,alikana kukutwa na mabomu  hayo kuomba mahakama kupunguzia adhabu hiyo.

Awali katika kesi hiyo Mwendesha mashitaka wa polisi upande wa Jamhuri  Athumani kisango ,aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe kufundisho kwa jamii na watu wenye kujihusisha na biashara  za kuuza siraha.

Mwisho 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply