sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » TFS KAHAMA YAKAMATA MBAO 2904 KWA WAFANYABIASHARA

Meneja wa  Huduma za Mazao ua Misitu Wilayani  kahama  Bruno Bahane 

 Mbao zilizokamatwa na wakala wa mistu na kamati ya ulinzi baada ya kufanya uperesheni katika mapoli ya ushetu  moyowos na mkweni  
  
 Baadhi ya milango ilikamatwa katika opereshine ya kamati ya ulinzi na wakala hao wa mazao ya mistu  

 Hivi ndivyo wa  wakala wa mazao ya mistu walivyokamata bajaji ikiwa na maguni ya mkaa 

Haya ni Magogo 74  ambayo yamekamatwa kwa kuvunwa bila ya kuwa na vibari vya kuvuna mazao ya mistu 

 Gunia 53 za Mkaa pamoja na pikipiki vikiwa vimekamatwa 

meneja wa wakala wa mazo ya mistu Bruno Bahane akonyesha mbao za ya elfu  ya efl mbili ionmbao 2904, 

 baadhi ya Magogo 

 Magogo akionyesha Meneja wa mazao ya misitu Bruno Bahane


KAHAMA
WAKALA wa 
 huduma za misitu  (TFS) Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kahama wamefanikiwa kakamata jumla ya mbao 2904 zilizokuwa zimevunwa na Wafanyabiasha wa zao hilo bila ya kuwa vibali husika na kuzihifandi katika maghala yao kinyume cha sheria.

  


Akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake juzi Meneja wa  Huduma za Mazao ua Misitu Wilayani hapa Bruno Bahane alisema kuwa Wafanyabiashara hao walikamatwa mwezi uliopita katika operesheni iliyojumuisha ofisi yake kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kahama.

Bahane alisema kuwa kazi ya Wakala wa huduma za misitu ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza rasilimali ya misitu  ya Serikali kuu ikiwa sambamba na kupanda miti kadri inavyohitajika katika jamii ili kutunza rasimilimali hiyo ya nchi isiwezekupotea kirahisi.

“Mimi kama Meneja wa huduma za Misitu tulifanya opereheni katika misitu iliyopo katika Wilaya ya Kahama pamoja na maghala ya wafanyabiashara wa mbao katika miji wa kahama kwa kipindi cha mwezi mei na kufanikiwa kukamata kiasi cha mbao 2904, Gunia 53 za Mkaa, pamoja na Magogo 74 na zoezi hili lilifanyika kwa mwezi mmoja”alisema.

Alisema kuwa ili kukabilina na watu walikuwa wakifanya Biashara hiyo bila ya kuwa vibali maalumu, walilazimika kushirikaiana na Kamati hiyo ya ulinzi na usalama katika kuvunja maghala ambayo yalikuwa yakihifadhiwa mizigo hiyo ya magogo ambayo yalikuwa hayana mihuri kutoka katika ofisi yake.

“Ndugu waandishi wa Habari mbao au magogo ambayo ni halali kwa mtu kuyamiliki yanatakiwa kuwa na mihuri kutoka katika ofisi yangu pamoja na nyaraka nyingine za kuambatisha lakini wafanya biashara hao walikutwa wakiwa na mapungufu kwa asilimia 100na hivyo kupelekea kutafisha  mizigo yao hiyo”alisema.

Hata hivyo Meneja huyo alisema kuwa mazao ya misitu sio biashara ambayo niharamu na kuwataka watu wafuate taratibu za kufanya bisahara hiyo na serikali haitachukua hatua yeyote kwa yule ambaye atakuwa hayupo kinyume na matakwa ya sheria ya mazao ya misitu.

Aidha Bahane alisema kuwa hali ya misitu kwa sasa sio nzuri kwani kumekuwa nauvamizi kwa watu kuingia na kufanya shughuli za kibinadamu kama kuendesha shughuli za kilimo, uchomwaji wa mkaa pamoja na ufugaji wa mifugo na kuwataka wananchi watoe ushirikinao na ofsi yake kwa ajili ya kuwabaini watu hao.

Hata hivyo Meneja huyo alisema kuwa misitu iliyoharibiwa kwa kiwango kikubwa ni ile ya kigosi Moyowosi, Mkweni,  na nyingine ikiwa katika Halmashauri ya ushetu pamoja na tabora ambayo shughuli za uchomwaji wa Mkaa, uchanwaji wa Mbao  pamoja na shughuli za kilimo zimekuwa zikifanyika kwa kiwango kikubwa.

  

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply