sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » HUYU Ndiye mh. Freeman Mbowe Kiongozi wa Chama cha Upinzani (CHADEMA) Nchini Tanzania Ninayemkubali

(1) Aliipasua CCM vipande vipande mwaka 2015 kwa kumfanya Lowasa kuwa Mgombea kiti cha Urais na kuufanya uchaguzi kuwa mgumu ktk historia ya nchi ya Tanzania Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya Kisiasa mwaka 1992.

Wafuasi wa CCM mamilioni waliamia CHADEMA na kwa tafiti za awali tu zinaonyesha bado wana hali ya kuja kumpigia kura za kutosha Lowassa mwaka 2020 na inaonyesha wengine watazidi kuiunga mkono CHADEMA maelfu ya wasomi Kutokana na kuitazama nchi kwa jicho la Tatu.

(2) Ndiye aliyekilinda Chama Cha Demokrasia Maendeleo(CHADEMA) kuwa chama Tishio kwa Chama Tawala (CCM). Vyama vingi vya upinzani Barani Afrika viliingiziwa vibaraka wa kisiasa na kuviharibu lakini si kwa CHADEMA ,,,mamluki na vibaraka huhama wenyewe au huumbuka kabla ya njama zao kutekelezeka na hatimaye kutimuliwa mapema .

(3) Ndiye kiongozi ambaye hanunuliki ,,hawezi kuwa kibaraka ndani ya mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania.Wanasiasa wengi wa Afrika hususani wa upinzani ni wanafiki na wasaliti huweza kununulika na vyama Tawala lakini si kwa nguli huyu wa siasa nchini Tanzania.

(4) Ndiye kiongozi anayetafutiwa kashifa ili akose credits za kuongoza CHADEMA na Taifa lakini imeshindikana. Mkumbuke kashfa za madawa ya kulevya . Ile kashifa ipo wapi ? Ikumbuke iliibua taharuki kubwa lakini sijaisikia tena.ILIPOTEA kama upepo .

(5) Ndiye kiongozi aliyewaandaa viongozi wengi wajao watakaopambana na Dhuluma na maonevu ndani ya Nchi mpaka nje ya mipaka ya Nchi .
Nikiwa kwenye Taasisi za Elimu ya juu mbalimbali nilishuhudia vijana wakipokea kweli zake kisiasa na kuwa wakakamavu wa hoja kupitia mikutano yake ya Kisiasa hususani anapofanya mikutano ya waandishi wa habari(Press conference ) kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na anapozungumza bungeni .

Kweli zake zimefanya wasomi wengi kufanya CHADEMA kuwa jukwaa halisi na la kuaminiwa ktk kuyazungumzia masuala ya Kitaifa hususani yanayolenga kuliondoa Taifa lilipokwamia mfano Kuwaletea wananchi wa Tanzania Maendeleo na kupigania haki zao dhidi wale wote wakandamizaji wa haki .

Kama mnasema Rais Magufuli ni mpigania haki za watanzania mnapaswa kujua kabla hajawepo Magufuli basi CHADEMA ulikuwepo na ndio imeibua kashifa zote za Mafisadi na wala Rushwa Serikalini bila kusahau Biashara ya madawa ya kulevya .

CHADEMA ikishirikiana na CUF ,NCCR mageuzi na wadau wa kupambana na Ufisadi iliibua kashifa za Mabehewa na vichwa vya Treni vibovu ,kashifa ya RADAR,MEREMETA ,ESCROW n.k .Kashifa zote Zilisimamiwa na kujadiliwa vilivyo chini ya Captain Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa vyama vya upinzani Bungeni.

(6) Ndiye aliyefanya kila mtanzania kwa asilimia kubwa kuwa Mwanasiasa na mwanaharakati na kuweza kupaza sauti dhidi ya wala rushwa na mafisadi .CCM kiujumla wanaweza kukataa lakini kuna wafuasi wengi wa CCM wamejifunzia kwa Mbowe ujasiri wa kusema ukweli juu ya Ufisadi na wizi wa fedha za Umma ulikuwa unaendelea Serikalini mfano masuala ya ESCROW, RICHMOND, Kashifa ya RADAR, Mishahara hewa,Wafanyakazi Hewa,Usafirishaji wa wanyama Hai nje ya Nchi n.k

(7) Ndiye kiongozi mvumilivu kisiasa Barani Afrika.Mara nyingi kauli zake zimeleta Mshikamano wa kitaifa badala ya kuleta matengano ya kitaifa. Hatakama kaonewa kajitahidi kuwa mwenye Hekima na Busara ktk kutetea haki zake .

(8) Ni mtu anayeitazama Tanzania kwanza badala ya CHADEMA. Ni mtu anayetazama watanzania kwanza kabla ya CHADEMA. Ni mtu wa mikakati kuliko maneno. Ni Simba wa mikakati ya kisiasa na kuthibitisha hilo Mtaona 2019-2020 mwaka 2015 mlishuhudia .

Mh.Freeman Mbowe kwa mwenye Akili Timamu hawezimpuuza hata Mara moja hususani ktk kuleta mageuzi MAKUBWA ya kiuchumi ,Kisiasa na kijamii . Kwa jamii ya kistaarabu na watu wasio na upendeleo Mbowe hapaswi kupuuzwa. Yote Niliyotaja HAPO juu Yana umuhimu mkubwa sana kwa Taifa letu.

Lakini nitaeleza umuhimu wa matukio au mambo mawili kwa kuwa mengine tajwa yamejieleza kiundani . Umuhimu nitakaoeleza ni wa matukio mawili ambayo ni kitendo cha kuigawa CCM vipandevipande na kitendo cha Mbowe kuilinda CHADEMA isiingiliwe na CCM . Twende pamoja ktk kuelezea umuhimu wa matukio hayo mawili,,,,,,,

(1) Kitendo cha Mbowe kuigawa CCM vipandevipande kwa kukubali Lowassa atumie jukwaa la kisiasa la CHADEMA kuwa mgombea Urais mwaka 2015 kuliifanya CCM ianze kujikagua na kuanza kujibadilisha mienendo yake kupitia baadhi ya viongozi wake na watendaji wa serikali Kuifanya nchi ya Tanzania kuwa shamba la bibi.

CCM ilijisahau sana HAPO hapana ubishi ,,,CCM iliamini Kuwa watatawala milele bila shaka 2015 waliamini sasa kwamba IPO siku watang'oka wakiendekeza mambo ambayo wananchi wa Tanzania hawayataki .Nakumbuka mwaka 2014 katibu mkuu wa CCM mh.Abuldulhaman Kinana aliwahi sema kuna mawaziri mizigo ktk Serikali ya awamu ya nne ,,,

sasa mawaziri hao hawa kuwa ni mizigo kwa maana ya vifurushi no walikuwa na kashifa nyingi za Ufisadi na wizi wa fedha za walipakodi masikini wa nchi hiii na kuna mawaziri wengine walisaini mikataba isiyo na tija kwa Taifa bila shaka walisaini kwa faida zao wao wenyewe.

(2)Kitendo cha MBOWE kuilinda CHADEMA isiigiliwe na CCM kama chama Tawala kumekifanya chama cha CHADEMA kuwa kioo cha kujitazamia kwa CCM na Serikali yake kwa miaka takribani 25 ya mfumo wa vyama vingi nchini tokea mwaka 1992 ,,,kwa maana ya kwamba ili CCM ijue imekosea au imepatia lazima itumie CHADEMA kama kioo chake cha kujitazamia ,,,,,na ndio kazi kubwa ya chama cha upinzani chochote chenye nguvu ktk nchi ya kidemokrasia.

Kauli ya Rais Magufuli ya hivi karibuni kwamba "Ukiona adui yako anakushangilia sana na kukusifu ujue umekosea na ukiona anakushambulia sana ujue umepatia''' inaonyesha wazi kuwa CHADEMA ni kioo kwa CCM na CCM inapaswa kuheshimu kioo hiki cha heshima Siyo kukiharibu .

Kioo cha kujitazamia ukikiharibu kuna wakati unaweza ukaenda nje ukadhani USO wako upo vizuri kumbe umebabuka ukatia aibu kwa watu nje.Kukipoteza chama cha CHADEMA ni faida kwa CCM na hasara kwa kitaifa kwani litakuwa likitembea gizani bila kujua nini kinaendelea ndani ya Serikali.

Daima nitasema kweli ,,Unafiki nitauweka kando kwa kuwa yapo maisha baada ya haya Duniani.

 CHADEMA haiwezi #potea kwa kuondoka kwa Madiwani wenye njaa.

 Kutaka kupoteza 
CHADEMA hakutaleta Maendeleo nchini Tanzania Bali ubunifu na utawala bora utaleta Maendeleo nchini.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply