sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » Polisi wazuia kusafiri Mfanyakazi wa Acacia uwanja wa ndege serikali imetoa maelezo.



Kampuni ya Acacia imesema kuwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kimataifa anayefanya kazi na Pangea Minerals Limited amezuiwa kuondoka Tanzania leo Julai 28 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya asubuhi.
Acacia wameeleza kuwa, mfanyakazi huyo ambaye hawakumtaja jina alikamatwa na hati yake ya kusafiria ilichukuliwa huku na yeye akishikiliwa kwa muda.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya kampuni hiyo, Acacia wamedai kuwa baada ya kuingilia sakata hilo kisheria, mfanyakazi huyo aliachiwa na hati yake ya kusafiria ikarejeshwa.
Aidha, wamesema tukio hilo limetokea kipindi ambacho kwa takribani siku mbili sasa wafanyakazi
wake wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa mbalimbali wa serikali.

Kuhusu tuhuma hizo, serikali kupitia kuwa Msemaji Mkuu, Hassab Abas imesema kuwa inafuatilia tuhuma hizo na baada ya muda mfupi watatoa taarifa kamili.
“Tunafuatilia ukweli wa madai ya Acacia kuwa mmoja wa maafisa wake amezuiwa kuondoka Tanzania.Tutatoa taarifa ya kina,” uliandika ukirasa rasmi wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa
Serikali.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply