JESHI LA ZIMAMOTO LATHIBITI MAJANGA YA MOTO NCHINI

 


Na Mwandishi wetu , Dodoma

Jeshi la zimamoto na uokoaji Limeshiriki Kuadhimisha Wiki ya utumishi wa umma Mkoani dodoma ambapo limesema lengo la kushiriki maadhimisho hayo ni kutoa elimu na taarifa pindi ambapo majanga ya moto hutokea.

Hayo yamesemwa Mkoani Dodoma na Naibu kamishina wa jeshi la zimamoto na uokoaji puyo Nzalayaimisi kwenye maadhimisho hayo ambapo amesema lengo kuu la kushiriki maadhimisho hayo ni kutoa elimu ya kudhibiti Majanga ya moto na uokoaji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati na kuchukua tahadhari.

Maadhimisho haya ya utumishi wa umma yanatukumbusha kuwa watumishi wote nchini kufanya kazi Kwa weledi hivyo Askari polisi tuna jukumu la kuhudumia jamii kwa wakati na uadilifu.

"Aidha Wizara ya mambo ya ndani kupitia jeshi la zimamoto na uokoaji tunawakaribisha Wananchi wote kutoka mikoa mbalimbali watembelee kwenye banda letu la zimamoto na uokoaji kupata elimu ya Uokoaji Wa mali pindi mafuriko ya majanga yanapotokea" Amesema Kamishina Nzalayaimisi

Post a Comment

Previous Post Next Post