Na Mohab
Dominick
Kahama
Oct 22, 2013.
MAHAKAMA kuu kanda ya Tabora iliyoketi Wilayani
Kahama Mkoani shinyanga juzi ilihairisha shauri namba 2/2012 la kosa la jinai
ililokuwa likiwakabili washitakiwa watatu la kosa shambulio la hatari lenye
kusababisha ulemavu wa kudumu kwa Kabula Nkalango (albino).
Kesi hiyo ambyo ilikuwa imepngwa kusikilizwa juzi
kwa mara ya kwanza na Jaji Sam Rumanyika
kutoka Mahakama Kuu Tabora inawakabili
washitakiwa Magobo Njige, Bupina Mihayo pamoja na Senga Mabirika.
Jaji Rumanyika alichukua maamuzi ya kuhairisha kesi hiyo baada ya
uapnde wa Washitakiwa kuwa na wakili mmoja ambaye ni John Ng’wigulila badala ya
kila mshitakiwa kuwa na wakili wake wa utetezi Mahakamani hapo.
Washitakiwa wote watatu wanathumiwa kwa kosa la
hatari kwa Mlemavu Kabula Nkalango Mlemavu wa ngozi (Albino) lililotendeka
katika kijiji cha Luhaga Wilayani Kahama mkoani shinyanga mwaka 2012.
Kushindikana kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kei
hiyo ya jinai kulidhaniwa kuwa wakili
mmoja angetosha kuwatetea washitakiwa hao lakini mambo yalienda tofauti kwa
watuhumiwa kutoelewana hali ambayo ilifanya mahakama hiyo isiweze kuoendelea
hadi wote watatu watakapopatikana.
Kutokana na sababu hiyo Jaji Sam Rumanyika
alililazimika kuhairisha kesi hiyo hadi tarehe 13/11/ 2013 ambapo kila
mshitakiwa katika kesi hiyo atakuwa na wakili wake kwa ajili ya utetezi pamoja
na mashahidi.
Mwisho.
No comments: