Na Mohab Dominick
Kahama
Oct 28, 2013.
KAURUGENZI wa Halmashauri tatu za Msalala na Ushetu
wametakiwa kuwanunulia Mahema Maafisa Ugani wake ili waende kupiga kambi katika
maeneo ya vijini kwa lengo la kumelimisha mkulima juu ya sula zima la kilimo
bora.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyasema
hayo juzi katika kikao cha ushauri cha maendeleo ya Wilaya ya Kahama
kilifanyika mjini hapana kugeza kuwa Afisa ugani kazi yake ni kupiga kambi
Vijijini.
Mapesya aliendelea kusema kuwataka maafisa Ugani hao
kuhakikisha kuwa wamapokuwa katika maeneo ya Vijijini wanawaelimisha wakulima
juu ya kilimo chenye tija wakulima husani wa zao la Pamba.
“Afisa Ugani kazi yake sio kukaa mjini lazima waende
Vijijini kuhamasisha Kilimo kwa Wakulima hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko
makubwa katika sekta nzima ya Kilimo katika Wilaya ya Kahama”, Alisema Mkuu
huyo wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya.
Aliendelea kusema kuwa anayetakiwa kukaa mjini ni Afisa
wa mapato tuu yaani wa TRA na kuongeza kuwa kwa Afisa ugani ni bora kabisa
akahamia kijijini kwa wakulima na kuwaongoza katika mambo mbalimbali yanahusu
Kilimo kwa wanaokuwepo.
Pia aliwataka Maafisa Ugani hao wawapo Vijijini
lazima wawe na mashamba ya mfano ya kuigwa na wakulima ambayo yatakuwa yametwa
vuzuri kulingana na kazi yao ya utaalumu wa Kilimo waliosmea.
Pamoja na Mambo mengine Mkuu wa Wilaya ya Kahama
aliwataka wakulima kubalika katika katika suala zima la kilimo cha kisasa na
kuongeza kuwa Mkulima apaswi kila msimu kukpoa tuu mbejeo lazima wabadilike.
“Mkulima unakuta katika mmoja wa Kilimo anapata
faida kubwa badala ya msimu mwingine kuacha kukopa na kutumia faida nayoipata
katika kununua Pembejeo yeye anahamia mjini kutumia fedha yake hali ambayo
msimu unafuata lazima akope tena”, Alisema Mpesya.
Aidha aliendelea kusema kuwa Serikali yake
imejipanga kumbadilisha mkulima awe mkulima wa kisasa zaidi kwa kuacha
kukopakop mara kwa mara na kutumia faida anayoipata kwa kununulia Pembejeo
katika msimu unaofuata hali ambayo wanaweza kuona faida ya Kilimo anacholima.
MWISHO
No comments: