Na Mohab
Dominick
0ct 28.2013
Kahama
Jeshi la
polisi wilayani kahama mkoani shinyanga ilimeteketeza jumla ya madawa ya kulevya mbalimbali ya aina
heroni,mirungi ,na bangi madawa haya
yalikamatwa maeneo tofauti katika wilaya ya kahama kwa kipindi cha January 2013
kwa mwaka huu.
Akisoma
taarifa hiyo kaimu mkuu wa polisi wilayani kahama Elis haway (Asp)kwa kiongozi
wa mbio za mwenge mwaka huu juma simai.alisema jumla ya kesi za madawa ya kulevya zimekamatwa
eneo la halmashauri ya mjini ni 17,watumiwa 62 walikamatwa ,na kesi 15
zimefikishwa mahakamani.
Adha haway akifafanua zaidi alisema kuwa kesi
9,zimefanikiwa na kesi 6,zipo mahakamani zinaendelea mahakamani na kesi 2,zinaendelea
na upelelezi.
Akifafanua
zaidi mkuu huyo wa polisi kuwa katika halmashauri za msalala na ushetu ambazo kipolisi zinahudumiwa na polisi wilaya ya kahama
zinaendesha msako katika maeneo yao na kupambana na madawa ya kulevya ,jumla ya
kesi 10,zimelipotiwa katika vituo vya polisi vilivyopo katika halmashauri ya kahama
na jumla ya watumiwa 19,walikamatwa,na kesi 8 zimefikishwa mahakamani na
kesi 5 zimepata mafanikio na kesi 3zipo mahakamani na kesi 2 zipo chini ya upelelezi.
Aidha kaimu mkuu wa polisi Elis Haway alisema kuwa
juhundi hizi zote zimetokana na mafanikio na mwitikio wa wanachi katika utoaji
wa taarifa za waharifu wa madawa ya kulevya na kuwezesha kukamatwa kwao.
Naye
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu alisema kuwa kwa sasa ongezeni
juhudi zaidi ziendelea kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kufanya misako ya pamoja na wilaya jirana na
wanachi walio wema kwa hili na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na hasa vijana kuhusu madawa ya kulevya na kuokoa taifa letu
kuwa na vijana walio adhirika na madawa haya.
mwisho
No comments: