Na Mohab
Dominick
Kahama
Oct 22, 2013.
MAMLAKA ya maji safi na Maji taka Kahama na
Shinyanga (KASHWASA) inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 1.7 na shirika la umeme
nchini Tanesco kutokana na kuchelewesha malipo ya bili za umeme unaendesha Mradi wa maji wa Ziwa victoria katika miji
hiyo miwili.
Hayo yalisemwa juzi na Meneja utawala na Rasilimali wa
Kashwasa Denis Mulingwa katika kikao Mkutano wa Taftishi wa wadau wa maji wa
kurekebisha bei za maji na huduma za mamlaka maji safi na usafi wa mazingira
Wilayani hapa (KUWASA)
Mulingwa alisema kuwa kiasi shilingi bilioni 1.3
serikali haijazitoa kama Ruzuku kwa mamlaka hiyo na hivyo kusababisha kuwawia
vigumu katika kulipa bili za umeme unaoendesha mradi huo mkubwa mkubwa kabisa
ulioigharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 254.
Aidha Mulingwa aliendelea kusema kuwa sasa Mamlaka
za Serikali hazina budi kubadilisha mfumo wa utendaji wa kazi kwa kutegemea
Ruzuku za Serikali kwani kwa kufanya hivyo kutafanya kazi nyingi kusimama hali
ambayo itazitia hasara mamlaka husika.
Alisema kuwa kwa Kashwasa imepata mfadhilia ambaye
atawakopoesha kwa ajili ya kuondokana na deni hilo na kuongeza kuwa wao
watatafuta mbinu nyingine za kuresjesha fedha hizo kuliko kusubiri Ruzuku hiyo
kutoka Serikali kwani kazi zitasimama.
Aidha Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa mashine moja
kati ya tatu katika mtambo wa kusafirisha mji kutoka katika chanzo cha Ihelele
imesimama na kuongeza kuwa kama hiyo moja nayo ikisimama basi huduma ya maji
inaweza kusimama hadi kuagiza vipuri hivyo kwa oda kutoka China au Afrika ya
kusini.
Katika Mkutano huo ambao ulijumuisha Wadau wa maji
wengi wao wakiwa wale wa matumizi ya nyumbani waligoma kupitisha mapendekezo
hayo ya kuongeza bei za maji na kuongeza kuwa mamlaka husika yaani kuwasa
itafute vyanzo vingine mbadala ya kuwaingizia fedha na sii mlaji wa maji.
Wakichangia katika mkutano huo Diwani wa kata ya
Kahama Mjini Abbasi Omary alisema kuwa mamlaka hiyo aiwezi kuongeza bei za maji
huku viongozi wake wakitumia fedha zaidi ya mamilioni katika suala la
mawasiliano pamoja na mafanyakazi anapofariki.
Alisema kuwa kutoka bei ya shilingi 595 hadi 970
ambacho kuwasa inataka kupandisha ni kikubwa na kuongeza kuwa bei hiyo hawezi
kumudu mwananchi wa hali ya chini kwani wao wanajukumu kubwa la kubuni vyanzo
mbadala vitakavyoisadia mamlaka hiyo na kuweza kujiendesha Mwenyewe.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka hiyo Joel
Rugemalila alisema kuwa katika mamlaka yake wametenga fedha hizo kwa ajili ya
mawasiliano pindi inapotokea bomba limefaribika sehemu na hivyo kupeleka huduma
mara moja na pia wananchi wanapotoa taarifa za wizi wa vifaa au kupasuka kwa
bomba.
M wisho
No comments: