Na
Mohab Dominick
Kahama
Oct
28, 2013.
KATIKA
kuhakikisha zao la Pamba katika Wilaya ya Kahama kwa mwaka ujao linamnufaisha Mkulima, Serikali Wilayani hapa
Mkoani Shinyanga imepiga marufuku
wakulima kutumia mbegu za manyoya na badala yake watumie mbegu kutoka katika
kampuni ya Quton.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alitoa ngalizo hilo katika kikao cha Kamati
ya Ushauri ya maendleo ya Wilaya ya Kahama kilichofanyika juzi Mjini hapa na
kuongeza kuwa Mkulima lazime alime kilimo chenye tija kwake kwa wakati huu.
Mpesya
alisema kuwa mbegu hizo kutoka Quton ambazo zinaitwa Delinted Seeds ndio kwa
sasa zenye tika kubwa kwa Mkulima tofauti na zile za Manyoya ambazo walikuwa
wakitumia hapo zamani.
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya aliendelea kusema kusema mbegu hizo zinauwezo wa kutoa kilo
1500, kwa heka moja na kuongeza kuwa kwa hali hiyo wakulima wanaweza kupata
kiasi cha pamba nyingi kwa kufuata wataalamu wa Kilimo watakaokuwa
wakiwaelimisha.
Aliwataka
Watendaji wa kata kuhakikisha kuwa Mkulima yeyote katika eneo lake hatmumii
Mbegu ya manyoya badala yake watumie mbegu hiyo mpya ambayo ileta mavuno mengi
na kuongeza kipato cha Mkulima na kutoa tahadhari kwa yeyote atakayetumia mbegu
za zamani apewe taarifa mara moja.
Mpesya
alisema pia mbali na mbegu hizo pia wanatarajia kwa mwaka huu Wakulima wa zao
la Pamba lazima walime Kilimo cha Mkataba na kuongeza kuwa mpaka kufikia hivi
sasa tayari wamwekishapata msaada wa mbegu kwa ajili ya kuzigawa kwa wakulima.
Alisema
kuwa kwa Serikali yake Imejipanga katika kuhakikisha kuwa Mkulima wa zao la
Pamba anapata faida kubwa kutokna na pamba yake anayolima na kuweza kumudu
ukali wa maisha ikiwa ni pamoja na kumudu kuendesha familia yake.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa kwa yale Makampuni ya makapuni ambayo
yatakuja ofisini kwake kwa ajili ya kuomba tenda ya kusambaza Pembejeo kwa
mwaka huu hayatayavumia kwani hayatapata kabisa.
mwisho
No comments: