Na
Mohab Dominick
Kahama
Nov
19, 2013.
WATUMISHI
UHAMIAJI SHINYANGA WAPATA MAFUNZO YA MAADILI YA KAZI.
WATUMISHI wa Serikali wametakiwa kuwa na utaratibu wa
kutunza siri za Serikali pamoja na kusimamia misingi , sheria na taratibu
zilizowekewa kwa lengo la kuleta ufanisi katika maeneo yao husika ya kazi.
Hayo
yalibainishwa juzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Halmashauri ya Msalala
Patrick Karangwa katika semina ya siku moja iliyojumuisha Wafanyakazi kutoka
katika Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ilifanyika Mji Kahama
Kalangwa
ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika semina hiyo alisema kuwa kwa sasa
ni wajibu wa Watumishi wa umma kufuata sheria na taratibu ili utendaji wa kazi
uweze kufanyika kwa ufanisi.
Aidha
Kalangwa alisema kuwa watumishi hao wa Serikali hususani wa Idara ua uhamiaji
lazima wajenge imani ya kuaminika na wateja wao wanaowatumikia hali ambayo
itaepusha malalamiko katika idara husika.
Pia
aliendelea kusema kusema kuwa kama mfanyakazi atakuwa anafanya vizuri katika
utendeji wake wa kazi hata nafasi zinapotokea za kwenda kujiendeleza atakuwa wa
kwanza kuchaguliwa kwa ajili jitihada alizozionyesha wakati wa kazi yake.
Awali
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga AnnaMaria Yondani alisema kuwa
lengo la Semina hiyo ni kukumbushana juu ya maadili ya Utumishi wa umma pamoja
na utunzaji wa Nyaraka mbalimbali za Serikali.
Yondani
aliendelea kusema kuwa Semina hizo zinazofanywa na Idara yake ni za mara kwa
mara ili kuwakumbusha watumishi wa Idara hiyo ya Uhamiaji juu ya Maadili ya
kazi pamoja na mambo mengine yanayohusu Idara hiyo.
Hata
hivyo alisema kuwa Semona hiyo inawajumuisha Watumishi wa iadara ya Uhamiaji
kutoka katika ofisi za Shinyanga, Isaka pamoja na Kahama na kuongeza kuwa ofisi
yake tayari imeunda kamati kwa ajili kusimamia nidhamu pamoja na mafunzo kama
hayo kwa ujumla.
mwisho
MGENI RASM MKURUNGEZI WA HALMASHAURI YA MSALALA PATRICK KARANGWA,KWA NIAMBA YA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA KATIKA SEMINA YA MADILI YA UONGOZI MJINI KAHAMA.
BAADHI YA WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA SHINYANGA NA KAHAMA WAKISIKILIZA MGENI RASMI MKURUNGEZI WA MSALALA HAYUPO PICHANI
BAADHI YA WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI WA WILAYA YA KAHAMA NA MGENI RASMI PATRICK KARANGWA MWENYE SHARTI NYEUPE NA MWISHO KULIA ALIKAA NI KAMISHA WA UHAMIAJI WA MKOA WA SHINYANGA ANNAMARIA YONDANI
No comments: