Na Mohab Dominick
Kahama
Nov 11, 2013.
MKURUNGEZI WA HALMASHAURI YA USHETU ISABELA CHILUMBA AKIWA OFISINI KWAKWE AKIJIBU SWALI ALILOULIZWA JUU YA TAFARANI YA WALIMU WAKE KATIKA KATA YA MPUNZE SHULE YA MSINGI YA IPONYANHOLO NA WAANDISHI WA HABARI AMBAO AWAPO PICHANI
WALIMUA wa Shule ya Msingi Iponyanholo kata ya
sabasabini Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametishia kuikimbia shule hiyo
kutokana na vitendo vinavyofanywa na Diwani wa kata hiyo Emanuel Makashi na
Mtendaji wa kata hiyo Elias Mpigamanoni kwa vitendo vya kuwalazimisha kuchangia shughuli za
maendeleo katika kata hiyo kwa nguvu sambamba na kuwaweka mahabusu.
Wakiongea na waandishi wa habari wa nipashe katika
kijiji cha mpunze Walimu hao walisema kuwa wamekuwa katika hali ngumu ya maisha
kutokana na Mtendaji wa kata hiyo wakishirikiana na Diwani wake kuwalamisha
kuchangia shughuli za maendeleo kiasi cha shilingi 28,500 na wengine walitoa
kiasi shilingi 10,000 katika kata hiyo wakati wanakatwa kodi katika
mishahara yao.
Walisema kuwa kwa sasa wamekuwa wakiishi maisha
magumu shuleni hapo na wanapowaona viongozi hao wakiwa na migambo wakija katika
shule hiyo walimu hao hulazimika kukimbia porini huku wanafunzi wakibaki
wakiwacheka hali ambayo wanafunzi wamekuwa wakiwadharau.
Mmoja wa Walimu hao Almachius Chereales alisema
kuwa tarehe 22/10/2013 alitumiwa Migambo
wawili waliokuwa na kamba na mawe mbele ya Wanafunzi na kuwekwa chini ya ulinzi
na kupelekwa katika Mahakama ya Mwanzo Mpunze iliyoamuru nikamatwe kwa kushindwa
kutoa michango ya maendeleo ya kata.
Mwalimu huyo aliendelea kusema kuwa aliwekwa
korokoroni kwa muda wa masaa 18 bila haya ya kupewa nafasi ya kujieleza hata
kumuona Mtendaji wake wa kata Mpingamanoni aliyedaiwa kuwa na kufungwa kwa
masaa hayo bila hata ya kupewa chakula kwa kipindi hicho.
Aidha Mwalimu huyo alisema kuwa Mtendaji huyo pamoja
na Diwani wa Kata hiyo Makashi wamekuwa
wakifika katika shule hiyo na kusema kuwa hawatambui mchango wa watumishi
hasahasa Walimu katika nchi hii na kuongeza kuwa mpaka Walimu hao wachange ndio
watakapowaelewa.
“Sisi Kama Walimu na Watumishi wa Umma hatukupewa
muda na Mwajiri wetu wa kuzalisha mali kwani mishahara tunayolipwa imebajetiwa
kwa Walimu na familia zetu kwa mwezi na
kuniingilia hivyo ni kama kunidhalilisha”, Alisema Mwalimu Chereales.
“Mshahara wangu wa kila mwezi unakatwa kodi ( Income
Tax) tofauti na Raia wa kawaida wasio wafanyakazi wa umma na pia bado kazi
ninayoifanya ni ya umma na hivyo nimecgania maendeleo ya Nchi yangu kwa
ujumla”, Aliongeza Mwalimu huyo.
Aidha aliendelea kutoa malalamiko kuwa alikamatwa
mbele ya wanafunzi wake kama mtu aliyevunja sheria kubwa za nchi na kuongeza
kuwa ili kushindwa kushiriki michango hiyo ni kuvunja sheria ipi?
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya
Kahama Simoni Edwini aliptakiwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo alisema kuwa
wao kama CWT wanafikiria juu ya kuifungulia
mashitaka Halmashauri ya Wilaya Kahama kwa vitendo vya udhalilishaji
wanavyofanyiwa walimu katika kituo hicho.
“Haiwezekani Mwalimu akakimbizwa mbele ya Wanafunzi
wake na kufungwa kamba kwa kosa la kutochangia maendeleo, leo mwalimu anweza
akawa kituo hiki kesho kingine je kila kituo anachopangiwa atakiwa akichangia
sehemu zote maendeleo”,Alisema katibu huyo wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kahama
Simon Edwin.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya ushetu
Isabela Chilumba alisema kuwa michango ya maendeleo kwa Walimu katika sehemu
husika si lazima lakini unaweza kuchangia kama kuna uwezekano.
“Mbona sisi Wafanyakazi huwa tunachangia katika
ujenzi wa sekondari na mambo mengine yaani hao walimu wameona nyinyi Waandishi
wa habari ndio mnaweza kuwatatulia matatizo yao?, Alisema Isabela Chilumba
Mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Mwisho.
No comments: