Na
CHOPA YA CHADEMA IKIWASILI KATIKA VIWANJA CHA MCHEZO CHA MPIRA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KWA AJILI YA KAMPENI YA PAMOJA DAIMA BAADHI YA WAKAZI WA KAHAMA WAKIMSIKILIZA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WIILBROD SLAA AKIWAHUTUMBIA WAKAZI WA KAHAMA KATIKA VIWANJA YA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA
KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILLBROD SLAA AKIWAHUTUMBIA WAFASI WA CHADEMA KATIKA VIWANJA VYA MICHEZO KAHAMA KATIKA KAMPENI YAO YA PAMOJA DAIMA
PIA MABANGO KAMA HAYA YALIKUWEPO
UMATI MKUBWA WA WANACHINI WAKIFURAHI HOTUBA YA KATIBU MKUU WA CHADEMA JANA MJINI KAHAMA
HII NDIYO CHOPA YA CHADEMA IKIWA IMESIMAMA BAADA YA KUTUA KATIKA VIWANJA VYA MICHEZO KAHAMA
BAADHI VIONGOZI WA KITAIFA WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)KATIKA JUKWAA KABLA YA KUANZA KWA MKUTANO WA PAMOJA DAIMA JANA MJINI KAHAMA
Jan 29,
2014.
KATIBU Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilbrod Slaa na Katibu Mwenezi wake
John Mnyika juzi wamemkataa Diwani wa Kata ya Majengo mjini hapa kupitia Chama
chao na kusema kuwa ni msaliti huku akituhumiwa na chama cha Mapunduzi katika
kukihujumu cha hicho.
Hayo yalisemwa
juzi na Katika mkutano wa Hadhara na katibu Mwenezi wa CHADEMA John Mnyika
wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Kahama katika moja ya mikutano ya chama
hicho ijulikanayo kama operesheni pamoja daima.
Mnyika alisema
kuwa katika chama chao hawatakubali kuwa na watendaji wasaliti na kwa sasa wapo
katika kazi ya kuwaondo watu kama Diwani huyo ambaye walimwita ni msaliti
mkubwa wa chama hicho na alipaswa kuondolewa kabisa.
Mnyika alisema
kuwa moja sababu zilizofanya Diwani huyo kuondolewa katika chama hicho ni madai
ya kuwa alishiriki katika kufanikisha Chama hicho cha Demokrasia na maendeleo
hakipeleki mgombea udiwani katika kata ya Ubagwe wilayani kahama ambapo
uchaguzi wa udiwani unatajiwa kurudiwa kutoka na aliyekuwa Diwani wa kata hiyo
Robert Mndula kufariki dunia mwaka jana.
Pia sababu
nyingine ni madai ya kuwa alikuwa akizunguka mitaani mitaani na kuwaambia watu
kuwa baadhi ya Viongozi wa CHADEMA walitoa kiasi cha shilingi milioni tano ili
kuwashinikiza wananchi wahudhurie katika mkutano huo ulifanyika juzi mjini
Kahama.
“Mimi ndie katibu
Mwenezi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo hapa nchini na Bobson ni
Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Kahama je, Wananchi unaniruhusu niondoke
Diwani huyo”, Alihoji Mnyika Katibu Mwenezi wa Chadema Taifa.
Kwa upande wake
Diwani wa Kata ya Majengo Bobson Wambura akiongea na Gazeti la nipashe akiwa
Jijini Mwanza kwa njia ya simu ya kiganjani kuhusu tuhuma hizo alisema kuwa
tuhuma hizo sii za kweli na wameamua kufanya hivyo kwa ajili msimamo wangu
Zitto Kabwe.
“Mimi bwana
Mwandishi Zitto Kabwe ni rafiki yangu iwe ndani ya chama au nje ya chama na
nipo tayari kwa lolote watakaloamua wenyewe mimi chadema sio yangu kwani hapo
zamani nilikuwa naishi kwa udiwani au chama?, Alisema Bobson Wambura Diwani wa
kata ya majengo.
Hata hivyo msafara
huo ambao ulikuwa ukiongozwa na John Mnyika pamoja na Dr, Slaa haukufanikiwa
kufika katika eneo la Ubagwe ambapo uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani
unatarajiwa kufanyika kutoka chopa walikuwa wakitumia kupotea njia na kutua
sehemu nyingine na hivyo kufanya safari yao kuihairisha.
Mwisho.
No comments: