Na
Kahama
Jan 24, 2014.
WADAU mbalimbali wa Elimu wakiwemo wazazi Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia Shule za
sekondari zinazomilikiwa na Wazazi baada ya shule hizo kuonekana zinapoteza mwelekeo kutokana na kukosa vifaa
mbalimbali vya kielimu.
Hayo yalisemwa juzi na Kaimu Meneja wa Shirika la
Hifadhi ya Jamii Mkoa wa Kahama ( NSSF) Ernest Rusato wakati akikabdhi Vitanda
80 na Magodoro ya idadi hiyo kwa Katibu wa umoja wa Wazazi wa CCM Wilayani
Kahama Sharon Tulliy kwa ajili ya kusadia katika shule ya sekondari ya Wigehe
inayomilikiwa na Wazazi.
Rusato alisema kuwa Shirika lake lilipokea maombi ya
msaada wa Vitanda pamoja na Magodoro kutoka kwa uongozi wa Wazazi wa CCM wenye
thamani ya shilingi milioni 30 lakini kusadia kwa kiasi kidogo wameamua kutoa
msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 10 vyote kwa pamoja.
Aidha Kaimu meneja huyo aliendelea kusema kuwa NSSF
mbali ya kujihusisha katika shughuli mbalimbali za kujenga uchumi hapa Nchini
pia wanajuhususha katika kutoa misaada mbalimbali hasa katika sekta mbalimbali
ikiwemo ile ya kukuza Elimu hapa nchini.
Pia aliwataka Wanafunzi wa Shule hiyo kpitia msaada
huo kuhakikisha kuwa wanasoma kwa bidii zaidi kwani wazazi wao wanajinyima kwa
kugharamikia karo za shule hali ambyo itawatia matumaini na hivyo kuweza
kutimiza ndoto zao walijiwekea hapo siku za baadaye.
Kwa upande wake katibu wa Wazazi wa CCM Wilaya ya
Kahama Sharon Tulliy alisema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwani shule
yake ilikuwa ikihitaji jumla ya vitanda 100 na kugeza kuwa sasa limebakia pengo
la vitanda 20 tuu katika shule hiyo ya Bweni yenye Wanafunzi 484 wa kike na
kiume.
Tulliy alisema Shule hiyo ambayo ni mali ya umoja wa
Wazazi Tanzania inatoa huduma za utaalamu na ina sifa nzuri pia haiendeshwi
kibiashara hali inayofanya kila mtoto mwenye kuwa na uwezo wa kusoma katika
shule hiyo bila ya kuwa na masharti yeyote yale.
Pia Tulliy aliwataka wadau wengine mbali na shirika
hilo la Hifadhi ya jamii kujitokeza kwa moyo katika kusadia shule hiyo ambayo
kwa ujumla baadhi ya wasomi wengi wa Wilaya ya Kahama wamesoma katika shule
hiyo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli pamoja na Jaji mstaafu
Hiema.
Shule ya Sekondari ya Wigehe ilianzishwa Mwaka 1954
kama shule ya ufundim kabla ya mwaka 1984 kuwa sekondari inahitaji msaada wa
haraka kutokana na uchakavu wa majengo yake pamoja na mabweni ya kulala
wanafunzi hali ambayo wadau na watu wenye mapenzi mema hawana budi kuisaidia shule
hiyo.
mwisho
No comments: