Na
Shinyanga
Febr 4, 2013.
HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO WILAYANI KAHAMA MH BRYARUGABA AKIWA NA ASKARI AFANDE THOMAS SIKU YA SHERI TANZANIA
BAADHI YA WANASHERI WAPONGEZANA KATIKA SIKU YA SHERI KATIKA VIWANJA VYA MAHAKANI WILAYANI KAHAMA
MAHAKIMU SHINYANGA WATOA KILIO CHAO KWA RC JUU YA
UKAMILISHWAJI WA JENGO LA MAHAKAMA KUU
UONGOZI wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga umemuomba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kuiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa
Mahakama Kuu ya Mkoa wa huo ili Mkoa
uweze kunufaika na huduma za Mahakama kuu badala ya kuendelea kufuata huduma
hiyo Mkoani Tabora.
Ombi hilo lilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama Mkoa wa
Shinyanga John Meseka katika Sherehe za maadhimisho ya siku ya Sheria Dunia
zilizofanyika viwanja vya Mahakama ya Mkoa Mjini Shinyanga.
Meseka alisema kuwa pamoja na Changamoto ya ukosefu
wa Mahakama kuu katika mkoa wa Shinyanga pia wanakabiliwa na uhaba pamoja na
uchakavu wa miundombinu hususani majengo
ya Mahakama ingawa mpaka sasa bado yanatumika katika shughuli nzima za
kimahakama.
Alisema jengo hilo la Mahakama kuu ambalo ujenzi
wake ulianza tangu mwaka 2008 lakini mpaka kufikia sasa bado jengo hilo
halijakamilika kwa matumizi ya shughuli
za kimahakama kuu kutokana na sababu nyingi ikwemo ukosefu wa fedha.
“Kwa maneno mengine tunakuomba Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Ally Rufunga uingilie kati
katika suala hili ili jengo letu liweze
kukamilika na Wananchi waanze sasa
kunufaika kwa kupata huduma ya Mahakama
Kuu katika Mkoa wetu wenyewe”Alisema
Hakimu John Meseka Chaba.
Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi Mfawidhi Seth
Mkemwa akitoa salamu zake alisema moja ya Vikwazo vinavyosababisha
ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama mbalimbali ni pamoja na ukiritimba
uliopo wa kimahakama na kuongeza kuwa ni bora mshitakiwa akasomewa mashitaka na
kesi yake ikasomwa siku hiyohiyo kama mashahidi watakuwepo wa kutosha.
Alisema kuwa Changamoto nyongine ni pamoja na
mashahidi kuwa na woga wa kutoa ushahidi katika kesi mbalimbali huku wakijua
kuwa Mahakama sio rafiki na watu wa kundi hilo hali ambayo inakuwa vigumua
katika kuendesha kesi mapema.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally
Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Mwanasheria kutoka katika
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Lightness Tarimo lisema kuwa uchelewashwaji
wa mashauri kufika kwa muda katika mahakama mbalimbali ni moja ya matatizo
yaliopo katika mkoa huu.
Alisema kuwa Mapango wa Matokeo makubwa sasa ni bora ukatumika katika ukamilishwaji wa
Jengo la Mahakama Kuu ya Mkoa wa
Shinyanga hali ambayo itapunguza mwendo mrefu wa kufuata huduma hiyo Mkoani
Tabora na kuongeza kuwa kwa mwaka huu wangefurahi kama sherehe hizo zingefanyika
katika jengo hilo.
Aidha alisema kuwa kwa sasa ataendelea kusisitiza
juu ya ujenzi wa Jengo hilo la Mahakama kuu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
Mahakama za Mwanzo ambazo pia zenyewe zimeonekana kuwa pungufu katika mkoa wa Shinyanga.
mwisho
No comments: