Na
Mohab Dominick
Bukombe
March 18, 2014
DIWANI APINGA
UANZISHWAJI WA MAENEO MAPYA YA UTWALA BUKOMBE.
MKUTANO maalumu wa
balaza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita
nusula ushindwe kufikia maazimio baada ya mmoj wa
Diwani kutoka katika chama cha Upinzani Soud Ntanyagara
(CHADEMA) Kupinga uanzishaji wa maeneo mapya ya utawala .
Mkutano huo
maalumu wa balaza ulioketi hivi karibuni katika ukumbi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe uliokuwa na lengo la
kupitisha mapendekezo ya uwanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala
ikiwa ni pamoja na vitongoji vipya, Vijiji pamoja na kata.
Akifungua
mkutano huo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
Felix Kulya aliwaarifu wajumbe kuwa ajenda
iliyopo katika Baraza hilo ni kupitisha mapendekezo
yaliyowasilishwa mbele ya balaza na si vinginevyo .
Alisema Agenda hizo
zilikuwa muhimu kupitishwa kwani mchakato ulikuwa umeanza na lilikuwa agizo
toka juu ambalo halikupaswa kujadiliwa bali kutekelezwa tuu na
baraza hilo la Madiwani .
Akichangia hoja
katika balaza hilo diwani wa kata ya Igulwa (CHADEMA)
Soud Ntanyagara alitaka kujua jografia na hali ya
uchumi katika Wilaya endapo inaweza kugharamia watendaji na
viongozi watakao hitajika katika maeneo hayo mapya
ikiwa hata yale yaliopo miundo mbinu yake ina sua sua.
Ntanyagara
alisema kuwa kwa sasa zaidi ya watendaji wa kata na vijiji
wapatao 40 wanafanya kazi kwa kujitolea katika ngazi husika pamoja na
hayo Halmashauri bado haijakamilisha ujenzi wa Zahanati
kwa kila kijiji na vituo vya afya kwa kila Kata.
Pia Diwani huyo
alisema kuwa baadhi ya vijiji havina shule za msingi na
sekondari pamoja na miundombinu ya mawasiliano yaani
barabara za kuunganisha kijiji na kijiji kata na kata na makao
makuu ya Halmashauri ya Wilaya hali ambayo inakuwa ni vigumu katika suala zima
la utekelezaji wake .
“ Tusijibebeshe
mlima wakati tumeshindwa kubeba kichuguu, hivyo nauliza
mwenyekiti hali ya mapato ya ndani kwa
Halmashauri yetu ikoje kwakuwa hata barua niliyonayo mkononi
ya wito wa balaza la leo imeonyesha mwendelezo wa
mazoea kwa waheshimiwa na wataalamu kukopwa posho za
vikao kwa maelezo kuwa Halmashauri ina hali ngumu
kimapato na iweje tushindwe kulipa posho ya madiwani
18 halafu tuongeze kata”, Alisema Diwani huyo.
Hata hivyo Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Kulya alitoa angalizo kuwa
haitakuwa sahihi kwenda kufanya mikutano na wananchi kupinga
mchakato huo kwa kuwa yalikuwa bado ni mapendekezo
ambayo.
Vuta ni kuvute
hiyo ilidumu zaidi ya masaa matatu mvutano kati
ya Soud Ntanyagara , Patric Kagulusi na Mwenyekiti wa
Halmashauri Joseph Kulya huku madiwani waliosalia wakipiga
meza kumsisitizia mwenyekiti kupitisha azimio.
MWISHO.
No comments: