sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA UZAZI WA MPANGO



Na  Mohab Dominick
Kahama
March 9, 2014.

WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA UZAZI WA MPANGO

AKINAMAMA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kujitokeza katika kupata Elimu ya  uzazi wa mpango kwalengo la  kuzaa watoto wachache wanaolingana na mahitaji ya familia wanazoishi ikiwa ni pamoja na kumudu gharama za kuwasomesha.

Hayo yalisemwa juzi na Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Emeleciana Machibya wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka kwa Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa Buzwagi katika sherehe za siku ya Wanawake Duniani.

Machibya alisema kuwa kwa jamii ya Kabila ya Wasukuma kwa kila kaya ina wastani wa kuzaa watoto nane na kuendelea hali ambayo inakuwa vigumu katika suala zima la kuwalea watoto hao pamoja na kuwapa Elimu.

Alisema kuwa katika usiku wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani jumla ya watoto 20 walizaliwa katika Hospitali idadi ambayo alisema kuwa ni ya kiwango cha juu kuliko hata Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ina idadi ndogo.

 Wakinamama wa Mgodi wa Afrikani Barrick God Mine  Buzwagi Wakiwa katika hospital ya Halmashauri ya mji wa kahama katika siku ya Wanawake Dunia Ambapo wakimama hao wa Godi huu Walikwenda kuwafariji wakimama Hospital hapo
 KAIMU mganga Mfawidhi Emeleciana Machibya Akiwa na kinamama wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi walipokwenda kutoa Zawadi Mbal;i mbali wakati wa madhimisho ya siku ya wanawake Duniani
 Baadhi ya wakinamama wa Mgodi wa Dhahabu wa Afrikani Barrick Godi Mine ya Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutoa Zawadi Mbali Mbali Zikiwemo Sabuni za uga ,Sabuni ya miche ,mabeseni ,pamoja na khanga
 AFISA  Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa buzwagi Salome Makamba Akiwa amepakata mtoto Ambaye Amezaliwa siku wa kuamkia siku ya wanaweke Duniani katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa kahama Ambapo wanawake wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi walikwenda kuwafariji wanawake wazao katika mahadhimisho hayo
 Mmoja wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Akiwa amebeba mtoto mchanga wakati walipokwenda hospital kutoa misaada katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa kahama
Moja wa wafanyakazi wa Mgodi wa  Dhahabu wa Buzwagi Akimpatia zawadi moja ya Mabeseni na sabuni Ambapo siku ya kinamama Duniani Ambapo uadhimishwa kila  mwaka tarehe 8,march 


Katika kuadhimisha siku hiyo ya Wanawake Wilayani Kahama Wanawake hao wanafanaya kazi katika Mgodi wa Buzwagi wakiongozwa afisa Mahusiano wa Mgodi huo Salome Makamba walitembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama na kutoa msaada vitu mbalimbali katika wodi ya wazazi kama vile Sabuni, Mabeseni, Kanga pamoja na vitu vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 1.7.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi Salome Makamba alisema kuwa wao kama Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi huo waliamua kujichangia fedha kwa ajili ya kusaidia wazazi hao ambao wengi wao ni wanawake wanaishi Vijijini wasiokuwa na uwezo.

Pia Makambali alishauru Wanawake wengine wenye mapenzi mema kujitokea katika kuwasaidia wazazi katika Hospitali hiyo kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri na kuongeza Kampuni hiyo ya Africna Barrick itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha akinamama wanasonga mbele.

Nae Mmoja wa Wanawake walioambatana katika msafara huo Mwajuma Ramadhani akiongea na Wanafunzi wa kike wa Shule ya sekondari ya Mwendakulima aliwataka wanawake kujiamini na kujiona kuwa wanaweza kufanya chochote na kuacha kuwa na tama na kuridhika na kila kitu wanachikipata.

Katika siku hiyo ya Wanawake Duniani Wafanyakazi hao wa Kike kutoka katika Mgodi wa African Barrick gold Mine inayomiliki Mgodi wa Buzwagi walitoa msaada huo kwa akinamama 45 na watoto 40 katika Hospitali hiyo pamoja na Madaftari kwa Wanafunzi wa kike 50 wa Shule ya sekondari ya Mwendakulima mjini Kahama.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

1 comments:

  1. mmm, wanawake wa Buzwagi ni wabunifu, watu na waige

    ReplyDelete