sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » FEDHA ZA KIGENI KATIKA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI NI KIKWAZO KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI HIZO.

   
MENEJA WA BENKI YA CRDB TAWI LA KAHAMA MR.LUTHER MNENEY AKIFUNGUA SEMINA HIYO.

IMEELEZWA kuwa Kutokuwepo kwa matumizi ya sarafu moja katika soko la pamoja la Afrika Mashariki kumeleta athari kubwa zitokanazo na matumizi makubwa ya fedha za kigeni katika nchi wanachama wa jumuia hizo.
Hayo yalieelezwa juzi na mwezeshaji kutoka makao makuu ya bank ya CRDB Ngeleja Mcharo katika semina ya wana hisa wa bank hiyo wilayani Kahama mkoani Shinyanga  yenye lengo la   kukuza uelewa wa soko la mitaji.
Mcharo alisema kuwa matumizi ya fedha za kigeni katika soko la mitaji la afrika mashariki yameleta changamoto hususan kwa wafanyabishara wanaofanya biashara katika nchi hizo.
Sambamba na hayo aliongeza kuwa uelewa mdogo katika masuala ya soko la pamoja pia ni changamoto ikiwa ni pamoja na baadhi ya sheria,kanuni,sera na vikwazo kutoondolewa katika muda uliopangwa.
Akizungumza kwa upande wa wafanyabiashara wa Tanzania Mcharo alisema kuwa wanashindwa kuhimili ushindani wa soko la pamoja kutokana na kutokuwa na mitaji mikubwa hali inayopelekea wafanyabishara wa nje kushikilia soko hapa nchini.
Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo walisema kuwa semina za elimu ya hisa ziwepo mara kwa mara ili kuwajengea uwezo zaidi wanahisa juu ya masuala ya kukuza mitaji .
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo Joseph Manyala alisema kuwa vikao vingi vya benki ya CRDB vinafanyika jijini Arusha hali inayofanya washiriki wengi kutoka sehemu za mbali kushindwa kuhudhuria.
Awali akifungua semina hiyo meneja wa benki ya CRDB tawi la Kahama Luther Mneney aliwataka wanahisa kuifanya benki ya CRDB kama mali yao na kwamba wazidi kununua hisa kwa faida zao na bodi ndiyo msimamizi.
Mneney alisema kuwa kwa sasa vijana wengi hapa nchini hawataki kuju mambo ya kibenki kama ya kukuza mitaji au mambo ya hisa halia ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na uelewa kuhusu mambo ya kibenki.
“Vijana wengi wameshika mambo mengi ambayo hayawasaidii katika maisha kama vile mambo ya mipira ya ulaya hali ambayo inawafanya kupitwana wakati na mambo ya kibeki na  watanzania  msiwe makarai kwa mitaji ya watu wengine”, Alisema Meneja huyo.
 MATUKIO KATIKA PICHA: 
MWEZESHAJI WA SEMINA YA WANAHISA KUTOKA MAKAO MAKUU YA CRDB DAR ES SALAAM MR NGELEJA MCHARO AKIENDELEA NA SEMINA HIYO ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA CARTAS MJINI KAHAMA.
 

WANAHISA WAKIWA KATIKA SEMINA

WANAHISA WAKISIKILIZA KWA MAKINI KATIKA SEMINA HIYO.

WADAU WA SOKO LA HISA WILAYANI KAHAMA WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO

WANAHISA WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO.

KATIBU MUHUTASI  WA BENKI YA CRDB TAWI LA KAHAMA GRORY LAUWO KUSHOTO AKIWEKA KUMBUKUMBU YA SEMINA.

WANAHISA WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO.

MUWEZESHAJI AKIENDELEA KUTOA MAFUNZO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply