sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » DIWANI KAHAMA MBARONI KWA KUFUNGA MLANGO WA OFISI ZA SERIKALI AKIMTAKA MTENDAJI KUONDOKA KATIKA KATA HIYO.

DIWANI WA KATA YA MWENDAKULIMA NTABO MAJHABI AKIWA CHINI YA ULINZI KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAMA.


Watu wawili akiwemo na Diwani wa kata ya mwendakulima wilayani kahama mkoani shinyanga Ntabo Majhabi jana wamekamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kufunga ofisi za serikali za mtendaji wa kata hiyo.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya mtendaji wa kata hiyo Cesilia Clement kupigiwa simu na mlinzi wa ofisi hizo Joseph Katambi na kumpa taarifa za tukio hilo liliofanywa na wananchi 15 walioambatana na diwani huyo.
Kwa mujibu wa mtendaji wa kata hiyo Cesilia Clement amesema kuwa waliamua kuibadirisha kamati ya sungusungu ya kata hiyo hali ambayo ilianza kuleta malalamiko na minong’ono ya chini kwa chini jambo lililoonyesha kuwa kuna watu walikuwa na maslahi na kamati hiyo.
Cesilia ameongeza kuwataja wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni pamoja na  Hamisi Abbas ambaye ni Fundi selemala na Makaka Benedicto wote wakaazi wa kata hiyo.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiongozana na kamati ya ulinzi ya kata na askari polisi walifika katika ofisi hiyo na kushuhudia jinsi mlango huo ulivyofungwa kwa kuwekewa kipande cha bati na kupigiliwa misumari tisa pamoja na mawe.
Aidhaa mkuu huyo wa wilaya alitoa amri ya kuvunjwa kwa bati hilo chini ya ulinzi wa askari polisi na kuamrisha wahusika wote waliofanya tukio hilo la kufunga ofisi za serikali ambazo zinahudumia wananchi kukamatwa akiwemo diwani wa kata hiyo.
Mpesya ameongeza kuwa kitendo hicho ni fedheha na kwamba ni jambo lisiloweza kuvumilika na kwamba ikiwa wamefunga ofisi ya mtendaji ipo siku watafunga ofisi ya mkuu wa wilaya kama sheria haitochukua mkondo wake.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata hiyo Cesilia Makula amesema kuwa kitendo hicho ni njama ambazo watu hawazijui na kwamba diwani huyo angetakiwa kufikisha malalamiko hayo ofisi ya mkurugenzi na siyo kuchukua maamuzi ya kufunga ofisi ya serikali.
Makula ameongeza kuwa watu hao waliofanya tukio hilo walikusanywa na diwani huyo kwa pikipiki na kwamba aliwaita waandishi wa habari ili kutoa taarifa hizo za kuifunga ofisi hiyo.
Awali Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mwendakulima Diwani huyo akiwa anawahutubia wananchi alimtuhumu Mtendaji huyo kujihusisha na hujuma za ajira katika mgodi wa Buzwagi ambazo hupitia kwenye ofisi yake.
Aidha amesema tuhuma zingine ni kuwaweka mahabusu wananchi wanaodai haki ya kusomewa mapato na matumizi ya michango yao hali ambayo Diwani huyo aliwataka wananchi wamuunge mkono kuifunga ofisi ili aondoke kufanya kazi kwenye eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka  jeshi la Polisi wilayani Kahama  Diwani huyo na wenzake wawili wanatarajia kufikishwa mahakamani siku ya jumatatu kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.
MATUKIO KATIKA PICHA:
HIVI NDIVYO MLANGO WA OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA MWENDAKULIMA ULIVYOFUNGWA NA DIWANI HUYO.


MAWE YAKIWA MLANGONI KUONGEZA KUFUNGA

MWONEKANO WA OFISI ZA KATA YA MWENDAKULIMA ZILIZOJENGWA KWA UFADHILI WA MGODI WA BARRICK
 
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA MWENYE SHATI JEUPE AKIWASILI ENEO LA TUKIO.
MKUU WA WILAYA AKIENDA KUSHUHUDIA JINSI MLANGO HUO ULIVYOFUNGWA.
MTENDAJI WA KATA YA MWENDAKULIMA CESILIA CLEMENT AKIONYESHA JINSI DIRISHA LILIVYOVUNJWA NA WATU HAO.

MKUU WA WILAYA AKIWA KWENYE MLANGO HUO AKIANGALIA JINSI ULIVYOFUNGWA KWA BATI.

MKUU WA WILAYA AKIWA AMESIMAMA PEMBENI AKISHUHUDIA FUNDI AKIFUNGUA OFISI HIYO.

FUNDI AKIENDELEA NA KAZI YA KUFUNGUA AMLANGO HUO.

ASKARI AKIWA AMEBEBA JIWE NA BATI HILO  BAADA YA KUFUNGULIWA ILI KUVIPELEKA KITUO CHA POLISI KWA AJILI YA USHAHIDI.

MSAFARA WA MKUU WA WILAYA UKIINGIA NDANI YA OFISI BAADA YA MLANGO KUFUNGULIWA.

MKUU WA WILAYA AKIWA NDANI YA OFISI HIZO.

MKUU WA WILAYA AKISAINI KITABU CHA WAGENI

MAKAMANDA WA SUNGUSUNGU WA KATA YA MWENDAJULIMA.

HAMISI ABBAS AMBAYE NI FUNDI SELEMALA ANAYETUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA DIWANI HUYO KUFUNGA MLANGO HUO AKIWA CHINI YA ULINZI.

MTUHUMIWA WA PILI MAKAKA BENEDICTO AKIWA CHINI YA ULINZI.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply