Na
Mohab Dominick
Kahama
May
25, 2014.
WAKULIMA
WA TUMBAKU KUWA BIMA
KAMPUNI
ya Real Insurance Tanzania Limited kwa kushirikiana na Benki ya CRDB iko mbioni
kutoa Bima kwa ajili ya Wakulima wa zao la Tumbaku Wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga kwa lengo la kuwafanya wakulima hao waweze kukopesheka katika
sekta ya Kilimo.
Akiongea
katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika Wilaya ya Kahama (KACU) Meneja wa
Kampuni hiyo Sodson Manatsa alisema kuwa Kampuni yake itatoa Bima hiyo ya kinga
ya majanga ya mvua, Upepo pamoja na mambo mengine kwa Mkulima.
Manatsa
alisema kuwa Wakulima wa zao la Tumbaku itakuwa ni muda muafaka wa kujiunga na
bima hiyo kwa Bei ya Chini huku kila Mkulima akitozwa asilimia 1.5 kwa ya
mavuno yake aliyoyapata kwa msimu ulipo wa zao hilo.
Alisema
kuwa hapo siku za nyuma wakulima walikuwa ni wagumu katika suala zima la kupata
mikopo kutoka katika asasi mbalimbali za kifedha kutokana na kutokuwa na kinga
yaani bima na kungeza kuwa kwa wakati huu itakuwa ni niia nyepesi kwao katika
kuchangamkia fursa za mikopo.
Hata
hivyo akiendelea kutoa maelezo juu ya bima hiyo Meneja huyo alisema kuwa katika
kuhakikisha Wakulima wa zao la Tumbaku wanakuwa ni bima hiyo ya mzao wataanza
kupita katika vyama mbalimbali vya msingi kwa nia ya kutoa Elimu na Semina ili
Wakulima waweze kujua faida ya kuwa na Bima ya mazao.
Alisema
kuwa suala hilo la Bima ya Tumbaku halitawahusisha Wakulima na Makampuni yao ya
ununuzi bali ni kwa Mkulima yeyote ambaye analima zao la Tumbaku jambo ambalo
wakitumia vizuri itawatoa katika wimbi la umasikini na kuweza kupata mikopo
sehemu mbalimbali.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Wilaya ya Kahama (KACU) Said
Tangawizi alisema kuwa wao kama Wakulima wa Tumbaku jambo hilo wamelipokea na
watalichukulia kama makisio na kisha kulitolea maamuzi baadaye.
“Suala
la kuanzishwa kwa Bima ya zao la Tumbaku sio baya kwa Wakulima bali
lisiangaliwe kwa upande mmoja na lisiingizwe katika utekelezaji kwa sasa ili
wakulima waweze kulitafakari wakati wakiwa wanapewa semina na Elimu juu ya Bima
hiyo”, Alisema Tangawizi Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Wilaya ya Kahama
(KACU).
Chama
cha Ushirika Wilaya ya Kahama juzi kilifanya mkutano wake Mkuu wa kumi na nane
wa mwaka kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ushirika huo ikiwa
ni sambamba na mapato na matumizi, faida na madeni mbalimbali yaliopo katika
ushirika huo ambapo unajumuisha Wajumbe kutoka katika Wilaya ya Kahama,
Bukombe, Biharamulo, Chato pamoja na Geita.
Mwisho.
No comments: