sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » CRDB YASAIDIA MADAWATI SHULE YA MSINGI MALUNGA

 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi malunga Akiwakaribisha wangeni toka bank ya crdb na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kahama katika makabidhiano ya madawati ambapo yamefadhiliwa na bank ya crdb ya mjini kahama
 Afisa Elimu ya msingi halmashauri ya mji Aluko Aluko Akitoa pongezi kwa Bank ya CRDB Wakati wa kukabidhiwa madawat jumla ya madawat( 20) ishirini yenye dhamanu ya shilingi milioni moja na ishirini Elfu
 Baadhi ya madawati yalitolewa na Bank ya CRDB ya mjini kahama katika shule ya msingi malunga Ambapo madawati hayo yana dhamani ya shilingi milioni moja na Elf ishilini jumla ya madawati(200)


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa kahama Felix kimaryo akitoa pongezi wa meneja wa Bank ya CRDB Mwenye tai nye ufito mweupe kati Luther mneney
 Meneja w Bank  ya CRDB mjini kahama  Luther  mneney Akiotoa maelekezo juu ya maendeleo ya shule zetu wachangia madawati kiasi hicho kidogo
 Meneja wa CRDB Mwennaye shati nyeupe Akimkabidhi Mkurugenzi wa mji Baadhi ya madawati Ambayo Bank ya CRDB Imetoa kwa shule hiyo ya malunga mjini kahama Ambapo jumla ya madawati 20 nyenye dhamani ya shilingi milioni moja na elfu ishirini
 Baadhi ya  wanafunzi na mkurugenzi  wa halmashauri ya mjin wa kahama ambaya yupo kati ya wanafunzi Felix kimaryo katika shule ya msingi malunga
Baadhi ya Walimu wa shule  ya msingi malunga wakiwa na maofisa wa wa Bank ya CRDB Katika picha ya pamoja shuleni hapoNa  Mohab Dominick
Kahama
May 27, 2014.

CRDB YASAIDIA MADAWATI SHULE YA MSINGI MALUNGA

BENKI ya CRDB Tawi la Kahama Mkoani Shinyanga juzi ilitoa Msaada wa Madawati 20 yenye thamani ya shilingi milioni moja  katika shule ya Msingi ya  Malunga Wilayani hapa ili kuwanusuru kundi kubwa la Wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wakiwa wamekaa chini.

Akitoa Msaada huo katika shule hiyo juzi Meneja wa CRDB Tawi la Kahama Luther Mneney alisema kuwa Benki yake imeamua kutoa kiasi kidogo walichonacho ili kuwanusuru Wanafunzi hao baada ya kuletewa ombi na Mratibu wa Elimu wa Kata hiyo John Tumbo.

Mneney alisema kuwa katika Benki ya CRDB ni kiasi cha asilimia moja tuu hutolewa kwa ajili ya kusaidia huduma katika jamii na kiasi hicho hugombaniwa na asasi mbalimbali zinazohitaji misaada hali ambayo inafanya benki hiyo kuchangia katika sekta tofauti tofauti kila mwaka.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa Tatizo la upungufu wa Madawati katika shule za msingi ni kubwa  haliwezi kuisha  bila ya kushirikiana wadau mbalimbali ili kuweza kuwasaidia Wanafunzi ili waweze kutimiza ndoto zao za baadaye walizojiwekea.

Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Aluko Aluko akipokea Madawati hayo alisema kuwa tatizo la Madawati katika Halmashauri ya Mji wa Kahama ni kubwa na kuongeza kuwa mahitaji ya Madawati katika shule hizo ni 15,630 wakati kiwango cha madawati yalipo ni 9,320.

Aidha afisa Elimu huyo aliendelea kusema kuwa kitendo cha Benki ya CRDB kuonyesha nia ya kusadia katika shule hizo ni kitendo cha kuigwa na Wadau mbalimbali wa Elimu ili kupunguza tatizo hilo na kama sii kulimaliza kabisa katika Halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Felix Kimaryo alisema kuwa aliwataka Walimu katika shule hiyo ya Msingi Malunga kuhakikisha kuwa madawati hayo yanatunzwa vizuri ili yaweze kuwasaidia na wanafunzi wengine ambao watasoma katika shule hiyo.

Alisema kuwa mbali na Benki ya CRDB kutoa msaada huyo Halmashauri yake Mji pia imetenga bajeti kwa ajili ya kutatua tatizo hilo la Madawati na hivyo muda sii mrefu hali hiyo ya upungufu wa madawati katika shule za Msingi katika Halmashuri ya mji wa Kahama litatoweka kabisa.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply