sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » KACU KUTONUNUA PAMBA MSIMU HUU WA 2014/2015



Na Mohab Dominick
Kahama
May 27, 2014.
 Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika kacu  mwenye kipasa sauti saidi Tangawazi katika mkutano mkuu wa kumi na nne wa chama hicho.
 Wajumbe wa chama kikuu cha ushirika kacu wakiwa katika mkutano wao wa kumi na nne wa chama hicho mjini kahama
 Afisa ushirika mkuu wa tume ya maendeleo ya ushirika ofisi ya mrajisi Dodoma Moshi Chogera wakati wa mkutano mkuu wa chama cha ushirika kacu mjini kahama ambapo ndiyo alikuwa mgeni mrasmi katika mkutano huu wa kumi nane mwenye kofia ni moja wa wajumbe wa mkutano huo wakijandili mambo mbalimbali .
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya ushetu isabela chiluba akiwa makiwa wakati wa kusomwa taarifa ya mkutano mkuu wa chama cha ushirika kacu katika mkutano wao wa kumi na nne wa chama hicho mjini kahama .
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ushirika kacu wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa chama hicho cha ushirika saidi tangawizi ambaye hayupo pichani wakati wa hotuba yake ya ushirika huo


Afisa ushirika mkuu moshi chogero aliye jishika kiuno akiwa na afisa ushirika wa mji mwenye kofia marco nzingula na mwenye shati jekundu ni mwandishi habari wa gazeti la majira wilayani kahama patric mabula wakimbadilishana mawanzo juu ya mkutano huo wa kumi na nne wa chama hicho cha kacu mjini kahama 


Na Mohab Dominick
Kahama
May 27, 2014.



KACU KUTONUNUA PAMBA MSIMU HUU WA 2014/2015

CHAMA cha Ushirika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga (KACU) kimesema kuwa hakitajihusisha na ununuzi wa wa zao la Pamba kwa msimu mwaka 2014/2015 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni hasara kubwa inayopata   pamoja na uzalishaji mdogo wa zao hilo kwa Wakulima wake.

Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa Chama hicho Said Tangawizi katika Mkutano Mkuu wa kumi na nane wa  KACU ulijumuisha Wajumbe mbalimbali wa vyama vya msingi kutoka katika Wilaya za Bukombe, Geita, Chato Pamoja na Wilaya ya Kahama.

Tangawizi alisema kuwa moja ya Changamoto zilizfnaya Chama hicho cha ushirika kuacha kununua Pamba kwa msimu huo ni pamoja na uzalishaji mdogo wa zao hilo na ushindani mkubwa kutoka kwa makampuni yanayofanya biashara ya ununuzi wa Pamba kutoka kwa Mkulima.

Alisema kuwa Changamoto nyingine ni gharama kubwa za uendeshaji wa Chama hicho huku gharama za uendeshaji kuwa kubwa na hivyo kukiacha chama hicho cha ushurika kuwa na Madeni makubwa kutoka katika taasisi za kifedha hususani Benki ya Benki ya Maendeleo Nchini (TIB).

Alisema katika ununuzi wa zao la Pamba kwa mwaka 2013/2014 Chama chake kilinunua kiasi cha kilo 541,713 za pamba kutoka Wakulima kiwango ambacho ni cha chini na kungezza kwa mwaka huu itabidi chama hicho kikae chini na kuangalia mambo mengine mablimbali ikiwa ni pamoja  na kulipa Deni kutoka TIB kwa kutumia vyanzo vya mapato walivyonavyo.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa pia chama chake kina mipango mingi ikiwa ni pamoja na kukaa na kupanga mikakati ya kilimo cha Pamba kwa kutumia Utaalamu zaidi ilivyokuwa ikifanya hapo awali jambo ambalo Chama hicho kilikuwa kikipata hasara katika manunuzi yake.

Akizungumzia kwa Upande wa zao la Tumbaku Tangawizi alisema kuwa katika msimu wa mwaka 2013/2014 jumla ya kilo 7200 ziliuzwa na wakulima kujipatia kiasi cha Dola la Kimarekani 164,547.35 katika msimu huo  huku pato Wastani kwa Mkulima ikiwa dola 2.2127 kwa kilo ta Tumbaku.

Alisema kuwa Kipato hicho kikubwa kilichangiwa na bei nzuri ambayo ilikuwa ikitolewa na Makapmpuni ya ununuzi wa Tumbaku  na hivyo kuwafanya hata Wakulima kuwa na uwezo wa kurudisha Mikopo yao katika Mabenki kwa Wakati uliopangwa.

Pia Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa pamoja na mafanikia katika zao hilo la Tumbaku pia kuna changamoto nyingi ikiwa ni pamoka na wakulima kutorosha Tumbaku na kuuza katika Makampuni tofauti pamoja na suala zima la ulanguzi  wa Tumbaku.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply