sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » HALMASHAURI YA MSALALA KUANZA KUPIMA VIWANJA



HALMASHAURI mpya ya Wilaya ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ipo mbioni kuanza kuyapima maeneo ya viwanja vya miji midogo kwa kupitia program za Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ardhi watakapokuwa katika mafunzo kwa vitendo kutokana na kupungukiwa wataalamu wa idara hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Zabron Donge aliyasema hayo wakati akijibu swali kutoka kwa Diwani wa Viti maalumu kutoka kata ya Kakola Asha Binde kutaka kujua kwamba mji huo utapimwa lini baada ya malalamiko mengi kutoka kwa Wananchi.

Donge alisema kuwa Halmashauri ya Msalala kwa sasa Haina Wataamu kwa kuweza kupima maeneo ya mji midogo hususani katika kata ya Kakola badala yake wameo Wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Ardhi kuwasaidia katika zoezi hilo pindi wanapokuwa katika mafunzo ya vitendo.

Alisema kuwa baada ya kutuma ombi hilo lilikubaliwa na kuongeza kuwa sasa wanasubiri Wanafunzi hao watakapoanza mafunzo kwa vitendo waje katika Halmashauri ya Msalala na kupima Viwanja katika mji midogo yote iliyipo katika Halmashauri hiyo.

Awali Diwani wa Viti Maalumu kutoka katika kata ya Kakoila Asha Binde alisema kuwa kwa sasa Wananchi wamekwisha changishwa kiasi cha shilingi 35,000 kwa ajili upimaji wa Viwanja lakini hadi kufikia hivi sasa bado hawajapimiwa hali inayowatia wasiwasi.’’

“Kama Halmashauri imedhamia kuleta Wanafunzi kutoka katika Chuokikuu cha Ardhi kwa ajili ya zoezi la upimaji ni bora zile fedha walizochangishwa hapo awali kwa ajili ya zoezi wakarudishiwa ili waweze kufanyia mambo mengine”, Alisema Asha Binde.

Aidha Diwani huyo alilaani kitendo cha kiongozi mmoja kutoka katika kata hiyo kuwachangishaw Wananchi hao kiasi cha shilingi 35,000 kwa ajili ya umimaji wa viwanja badala ya shilingi 30,000 hali ambayo ilimfanya kupata kiasi cha zaidi ya shingi milioni moja hali ambayo ni wizi wa kauminika.

“Huyo kiongozi wa Serikali aliwachangiasha Wananchi shilingi 35,000 badala ya shilingi 30,000 huku akiwaibia shilingi 5,000 kwa kila Mwananchi nab ado anafanya kazi katika Halmashauri ya Ushetu baada ya kukimbia Halmashauri ya Masalala tunakuomba Mkurugenzi Mtumishi huyo aweze kuwajibishwa ili arudishe fedha hizo”, Alisema Diwani huyo.

mwisho


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply