sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » TBL KUUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA MAUWAJI YA TEMBOKAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imesema kuwa itaendelea kuungamkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupambana na winmbi la majangili wanaouwa Tembo hapa nchini hasa kwa kupitia bia yake ya Ndovu.

Hayo yalisemwa juzi na Afisa Tarafa ya Msalala Addy Mtaule wakati wa sherehe iliyoandaliwa na Kampuni hiyo ya bia iliyojumuisha wadau mbalimbali wa Kampuni hiyo na wauzaji wa bia katika mji wa Kahama kwa ujumla .

Mtaule aliyasema hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambaye alikuwa Mgeni Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo na kuongeza kuwa Serikali itakuwa bega kwa bega n a Kampuni hiyo

Alisema kuwa kwa sasa hapa nchini kumekuwa na wimbi kubwa la mauwaji ya Mnyama Tembo huku majangili hao wakichukua Pembe zake na kwenda kuuza katika nchi mbalimbali kwa lengo la kutafuta utajiri wa haraka.

Awali akitoa Salamu za TBL Meneja Mauzo kanda ya ziwa Sylivester Syzya alisema kuwa lengo kubwa la kufanya sherehe hiyo ni kufahamiana na kuongea mambo mbalimbali yanayohusu biashara hususani zile bidhaa zinazotengenezwa na Kampuni hiyo pamoja na wateja wao.

“Tuna muda mwingi hatujawakutanishja wateja wetu kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza kuhusu nini tufanye sisi kama Kampuni ya biasha na ni nini kimepungua ili tuweze kuboresha hasa katika bia ya Ndovu”, Alisema Syzya Meneja mauzo kanda ya ziwa.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa Kampuni hiyo itaendelea katika kuwajali Wateja wake katika mambo mbalimbali ya kuboresha biashara zao ili waweze kutimiza malengo yao la kuwa na mitaji mikubwa itakayowasadia katika kupanua wigo wa biashara.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply