sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MADIWANI WAGOMA KUONGEZEKA KWA GHARAMA HOSPITALI YA WILAYAMADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya msalala wamepinga Mapendekezo ya kitengo Idara ya Afya kuongeza kiasi cha fedha za huduma za papo kwa papo kutoka kiasi cha shilingi 1,000 kilichokuwepo hapo awali hadi kufikia kiasi cha shilingi 7,000 kwa lengo la kuchangia mfuko wa afya ya jamii (CHF).

Diwani wa viti Maalum (CCM) Angela Paulo kutoka kata ya segese alikuwa wa kwanza kupinga mapendekezo hayo yalioletwa katika Baraza la Madiwani na  Kaimu Mganga Mkuu wa Haspitali wa Halmashauri hiyo Charles Kalidushi na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo ni kama kumuongezea Mwananchi mzigo.

Paul alisema kuwa kwa sasa Wananchi wanashindwa kumudu kuchangia huduma ya shilingi 1,000 katika kupata huduma Hospitali ya Wilaya na kungeza kuwa kwa kitendo cha kungeza fedha hiyo kutawapa shida wananchi na kunaweza kuchangia kuongzeka kwa vifo hasa kwa akinamama.

“Kitendo cha kuongeza malipo ya huduma za papo kwa papo katika Hospitali ya Wilaya ni kitendo cha kumuongzea Mwananchi mzigo kwani hiyo ya awli tuu hawezi kumudu na mkifanya hivyo mnaweza kuongeza vifo hasa kwa jamii ambayo haina uwezo wa kumudu gharama hizo”, Alisema Angela Paul.

Aidha Diwani huyo alisema kuwa njia ya kuwafanya wananchi kuingia katika mfuko huo wa Afya ya jamii kwa kuwaongezea huduma hiyo ni bora wakaelimishwa kwanza kabla ya kujiunga na mfuko huo huku wataalamu wa Idara ya Afya wakishirikina na madiwani kupita katika kata mbalimbali kwa lengo la kuwashawishi wananchi juu ya mfuko huo.

Awali akitoa Mapendekezo hayo Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Masalala Charles Kalidushi alisema kuwa Idara ya afya imeamua kutoa mapendekezo hayo kwa madiwani hao ili  iwe rahisi kwa Wananchi kuchangia kiasi hicho cha fedha ili waweze kupata huduma wao na familai zao.

Kalidushi maliendelea kusema kuwa tayari watu wa idara ya afya wameishaanza kupita vijijini kwa lengo la kuwaelewesha wananchi juu ya umuhimu wa kuingia katika Mfuko wa Afya ya jamii na wananchi wameonyesha nia ya kuchangia kiasi hicho cha fedha cha shilingi 7,000 kwa mwaka.

Alisema kuwa kwa kupitia Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) Wananchi hawatakuwa na shida ya kupata Dawa katika Vituo vya Afya sambamba na kulipia kumuona daktari hali ambayo itakuwa rahisi kwa kupata huduma haraka na kuwahi kurudi majumbani kwao mapema kuliko ilivyokluwa awali.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply