Na Mohab
Dominick
Kahama
April 23, 2014.
WANANCHI Wilayani Kahama Mkoani shinyanga wamesikitishwa na vitendo
vinavyofanywa na Wajumbe wanaojadili
Rasimu mpya ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kitendo cha
kutoelewana katika majadiliano yao hali ambayo inafanya wakati mwingine baadhi
ya Wajumbe kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Wakitoa maoni yao na gazeti la nipashe Wananchi hao walisema kuwa kitendo cha wajumbe
wa Bunge hilo la rasimu ya katiba mpya kutoelewana kila siku kunasababisha hadi
wananchi kutokuwa na hamu ya kuliangalia kwa kuwa wanakuwa na wasiwasi kama
katiba ya nchi hii itapatikana kwa staili hiyo.
Wanasema kuwa kwa sasa wakati wananchi wa nchi nzima
macho yao yakiwa katika mji wa Dodoma kusikiliza Bunge hilo ni bora wakakaa kwa
utumilivu na kujadili rasimu hiyo bila ya kuwa na malumbano yeyote kwani kwa
zimebaki siku chache tuu za kujadili Rasimu hiyo lakini mpaka kuifikia hivi
sasa bado watanzania bado hawajapata jibu kuhusu majadiliano ya bunge hilo.
“Kwa sasa Wananchi wamekuwa hawana imani na Bunge
hilo linaloendelea Mjini Dodoma hali ambayo imefanya wengi wao hata kukata tama
ya kuliangalia kwani wanasema kuwa bunge hilo kwa sasa limekuwa tofauti na
watanzania walivyokuwa wakidhani litakuwa kwa manufaa yao”,Walisema Wanachi
hao.
Mmoja wa wananchi hao ambaye ni Diwani wa Kata ya
Bugarama Nickson Igoko alisema kuwa kwa sasa Wajumbe hao wa Rasimu ya Katiba
Mpya kukaa na kuelewana kwani jicho la Watanzania linawaangalia wao kwa sasa
ili kuweza kupata mustakabali wan chi yao kwa miaka 50 ijayo.
“Tukishindwa kujadili Rasimu hii ni kama kupoteza
Mwelekeo wa Watanzania hasa wengi wao wakiwa maeneo ya Vijijini ambapo hawajui
chochote kinachoendelea hadi sasa hali ambayo itakuwa ni kama kutowatendea haki
watu hao”, Anaongeza Nicksoni Igoko Diwani wa Kata ya Bugarama (CCM)
Alisema kuwa wakati wajumbe wa rasimu hiyo
wakichaguliwa watanzania wengi walikuwa na imani nao hali ambayo kwa sasa
imekuwa tofauti kwani kila siku kumekuwa na malumbano baina ya watu pande mbili
hali ambayo kwa sasa zimebaki siku 12 kusitishwa kwa bunge hilo bila ya kuwa
hata na mwelekeo hata mmoja kwa kupatikana kwa Katiba hiyo.
Igoko aliendelea kusema kuwa kusitishwa kwa Bunge
hilo bila ya kuwa na mwelekeo kwa kipindi cha miezi mitatu waliokaa ni kama
kuwatania watanzania ukizingatia kodi za Wananchi zinapotea kwa wajumbe hao
kulipwa posho kwa kipindi hicho hali ambayo inafanya wananchi kuwapotezea hamu
ya kuliangalia bunge hilo.
“Ni bora bunge hilo lingekuwa na watu 30 tuu ambao
wangekaa kwa kuelewana hali ambayo hadi kufikia hivi sasa wananchi wangekuwa
tayari wamepata picha ya katiba yao ingekuwa vipi kuliko kukalia kubishana bila
ya kuwa na mafanikio yeyote na kuwajengea watanzania hofu ya kupatikana kwa
katiba hiyo mpya”, Alisema Diwani huyo
mwisho
No comments: