Na Mohab Dominick
Shinyanga
May 29,2014,
WAJIFANYA MUNGU WATU KUENDESHA BARAZA LA ARDHI SHINYANGA
Wakazi wa kata ya Tinde katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini mkoani
humo wamelilalamikia baraza la ardhi la kata hiyo kwa kuwanyima haki zao
kutokana na maamuzi ya kesi kutotolewa kwa wakati kwa lengo la kijipatia
chochote.
Kauli hiyo imetolewa juzi na mmoja wa wakazi wa kata hiyo,Clement
Wiyeke wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti juu ya
baraza hilo kujingeuza kuwa mungu Watu kwa kutowatendea haki wananchi na
kutaka wapewa chochote.
Wiyeke alieleza kuwa wamekuwa hawafanyi kazi kama inavyotakiwa na
kwenda kinyume na Sheria ya Mabaraza ya Ardhi ambapo pia wamekuwa wakiangalia
ni mtu wa aina ipi aliyepeleka kesi pale kama ni mwenye pesa au la ndipo
wamshughuliki swala lake.
Hata hivyo akiongelea swala hilo mwenyekiti wa baraza la
ardhi, Kazumari Mnala Mkulunga alisema kuwa wao kama wasuruhishi wa migogoro ya
ardhi katika kata hiyo wanafanya kazi bila kuangalia mtu yeyote mwenyepesa au
hana pesa kama inavyodaiwa.
Mwenyekiti huyo alisema wanafanya kazi katika mazingira mangumu
kwani hata sehemu ya kuwekea majarada ya kesi hawana bali hujinunulia wao hali
ambayo inapelekea kwa baadhi ya mashauri kupotea na kuiomba halmashauri
kutowatelekeza kwa shunguli ngumu ambayo haina posho.
Mkulunga ameitaka serikali kuwaboleshea miundombinu na mazingira
ya kazi na kuwapatia walinzi kwa shunguli za maamuzi ya
mashauri zinapoendeshwa kutokana na baadhi ya watuhumiwa kuwa wakorofi na
wapate ajira ya kudumu kwa wenyeviti pamoja na makatibu kwa kuajiri watu mwenye
elimu ya Sheria.
MWISHO.
No comments: