Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya Akiangalia Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na kanisa la huduma ya mlima wa makimbilio mjini kahama
Mkuu wa wilaya ya kahama akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na wakuu wa idara mbalimbali za wilaya ya kahama wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa makabidhiano vifaa mbalimbali toka kanisa la huduma mlima wa makimbilio katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya kahama
Baba Askofu Rizik Esrom Akitoa maelenzo kwa waadishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya kahama baada ya kutoa misaada hiyo kwa mkuu wa wilaya ya kahama vifaa hiyo vina dhamani ya milioni 14.5
Katibu tawala wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya kahama mwenye karatasi mkononi julias mushi, kati ni mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya mwenye kitabu chekundu ni Baba Askofu Rizik Esrom wa kanisa la huduma mlima wa makimbilio
Baadhi ya wahuduma ya kanisa la huduma mlima wa makimbilio wakitoa vifaa mbalimbali kwenye magari kwa ajili ya kupelekwa kwa watoto yatima na wajane mjini kahama
Mmoja wa watumishi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya kahama alitambulika kwa jina moja tu la ungumba akisaidia moja ya mzingo iliyoletwa na kanisa la huduma la mlima makimbilio
Baadhi ni vifaa vya msaada toka kanisa la huduma mlima wa makimbilio vikiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya kahama leo
Na Mohab
Dominick
Kahama
May 29, 2014.
KANISA LATOA MSAADA KWA YATIMA NA WAJANE KAHAMA
ASKOFU wa Kanisa Huduma Mlima wa Makimbilio Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga Rizik Esrom juzi alitoa Msaada wa Nguo kwa Serikali ya Wilaya ya Kahama kwa
lengo la kusaidia akinamama wajane na Watoto Yatima waliopo Wilayani hapa.
Akitoa Msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama
Benson Mpesya, Askofu huyo alisema kuwa Kanisa lake limeguswa na kutoa msaada
huo na kuona ni muhimu sasa katika kuwatazama Mayatima na Wajane waliopo
Wilayani hapa.
Esrom alisema kuwa msaada huo pia umelenga Akinamama
wajane wasiokuwa na uwezo kabisa wa kufanya kazi hali ambayo itapunguza ugumu
wa maisha walionayo katika familia wanazoishi.
Askofu huyo alisema kuwa msaada huo una jumla ya thamani
ya milioni 14.5 na kuongeza kanisa lake halitaishia hapo katika kuchangia kwa
jamii isiyojiweza katika Wilaya ya Kahama na kuongeza kuwa huo ni mwanzo tuu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson
Mpesya akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali alisema kuwa msaada huo
umekuja wakati muafaka na kuongeza kuwa atawaita Maafisa wa Maendeleo ya jamii
katika Halmashauri tatu ili waweze kuona jinsi ya kuzigawa katika maeneo yao.
Mpesya aliwataka Makanisa mengine Wilayani hapa
kuguswa kama lilivyoguswa kanisa hilo katika kusadia katika shughuli za
maendeleo ya jamii hususani katika kuchangia watu wasiokuwa na uwezo kama
Watoto Yatima pamoja na Wajane.
Aidha alisema kutoa ni moyo na sio utajiri na watu
wa aina hiyo ni muhimu katika kuwasaidia ili na wao wajione kama watu wengine
na sii kuwaacha wapweke huku wakijua kuwa hawana msaada wowote katika jamii
inayowazunguka.
mwisho
No comments: