sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MADINI YA BATI YATOROSHWA KWENDA RWANDA


 vijana wake wamepumzika baada ya kazi ngumu katika machimbo hayo
 maji ambayo hufanyiwa uchejuaji wa madini ya tini ambapo hutunzaji wa maji huwekwa kwa huangalifu mkubwa
 moja ya shimo ambapo madini ya tin yatoka
 hii ni jengo ambalo afisa madini mkoa wa kagera amepatia muekezaji kujenge katika maeneo ya serikali kwa manufa yake binafsi
 hii ndiyo list feki ilitoliwa na ofisi ya madini mkoa wa kagera ikiwa na mhuli wa serikali
 afisa madini wa mkoa wa kagera arbogast kalist akiaonyesha list feki toka kwa waandishi wa habari ofisini kwake
 afisa madini wa mkoa wa kagera arbogast kalist akionyesha kitabu kwa waandishi wa habari kuhusu tuhuma za kuwalinda wananchi wa nchi jirani ya rwanda ofisi kwake
                                                                            eneo la machimbo
                                   haya ndiyo madini ya tin (bat)
 moja ya jengo la stamico ambapo afisa madini wa mkoa amepangisha rai wa rwanda
 mmoja ya wachimbaji wa madini ya tin (bati)haruna wabulungu mkazi wa rwanda jina marufu mkoma simba  akiwa ameshika madini  hayo 
 baadhi ya wanyarwada wakiwa eneo la machimbo ambapo inasemekana kuwa ndiyo wachukuwa madini hayo katika kijiji cha sindiketi ambapo majini yao hayakutambulika mara moja
 hili ndiyo shimo ambapo linatoka madini ya tin (bati)
 baadhi ya majengo ambayo yalikuwa ni ofisi za stamico wilayani kyrewa mkoa wa kagera ambapo upande wa kulia afisa madini wa mkoa wa kagera mkupatia muekezaji kujenge nyumba eneo hilo
 eneo la machimbo ya madini ya tin ambapo mazingira kama jinsi yanavyo alibiwa na uchimbaji huo
 baadhi ya mitambo ya waakezaji ya uchimbaji wa madini ya tin wilayani kyrewa ambayo mkuu wa wilaya ya kyrewa mpaka hapo mikataba yao itakapoiona kutokana na wanachi kuchukuliwa maeneo yao na kulipwa fedha kiasi bila ya makumbaliano na hao wananchi na wengine kukataa malipo hao
 vijana wadogo ambao wapo eneo la machimbo ya tin (bati)wilayani kyrewa mkoa wa kagera
 baadhi ya majengo ya stamico ambapo afisa madini wa mkoa wa kagera ameruhusu muwekezaji kujenga jengo hilo eneo la serekali
 afisa madini wa mkoa wa kagera arbogast kallit akiwaonyesha moja ya list za serikali kuhusu tuhuma ya kuwa na list feki ofisini kwake
 baadhi ya wachimbaji  wa madini ya tin (bati)wakiwa katika kusubiri wenzao walioko chini ya mashimo wakiwasubiri
 nyumba za wachimbaji wa madini ya tin mkoani kagera wilaya mpya ya kyerwa


 maeneo la makazi ya wachimbaji wa madini ya tini mkoani kagera wilaya mpya ya kyerwa




Na   Mohab Dominick

Kyerwa BUKOBA
Juni 20, 2014.

MADINI YA BATI YATOROSHWA KWENDA RWANDA

WANANCHI   wa Wilaya mpya ya Kyerwa Mkoani Kagera wameiomba Serikali kudhibiti Madini ya Til (Bati) yanayochimbwa katika Wilaya hiyo kutokana na baadhi ya Viongozi wa Madini Mkoani hapa kushirikiana na Wanyarwanda katika kuyatorosha Madini hayo kwenda nchi ya jirani ya Rwanda.

Wakiongea na blong hii Wananchi hao walisema kuwa wamekuwa wakishangazwa na wimbi la Watu hao kutoka katika nchi ya jirani ya Rwanda kumimini katika mchimbo hayo kwa kudai kuwa hapa nchini hakuna soko wala mitambo ya kusafishia madini hayo ya Bati.

Walisema kuwa sehemu hiyo maarufu kwa jina la syndicate hapo siku za nyuma ilikuwa ikimiliwa na shirika la kutetea Wachimbaji wadogowadogo (STAMICO) kwa sasa limevamiwa na Wanyarwanda na kujimilikisha maeneo mbalimbali ya uchimbaji huku Watanzania wakinyimwa fursa hiyo na ofisi ya Madini Mkoa.

Mmoja wa Wanyarwanda hao ambaye yupo katika machimbo hayo tangu siku za nyuma Wabulungu Haruna alisema kuwa ofisi ya Madini Mkoa wa Kagera imekuwa ikitoa Vibali vya uchimbaji wa Madini hayo ya Bati kwa Wanyarwanda  huku akisingizia kuwa hakuna mtanzania anayeweza kufanya biashara hiyo kwani hapa nchini hakuna sehemu yenye mitambo ya kusafishia madini hayo.

Haruna alisema kuwa Madini hayo ya bati katika eneo hili yalikuwepo tangu siku za nyuma chini ya STAMICO lakini baada ya shirika hilo kujitoa ndipo Wanyarwanda hao walipoamia katika Kijiji hicho na kusingizia kuwa soko kubwa la Madini ya Bati lipo katika nchi ya Rwanda na sii Tanzania na hivyo kuwafanya wazawa kubaki kuwa madalali tuu.

“Tunaomba ofisi za uhamiaji Mkoa wa Kagera kuja katika eneo hilo kwani Wanyarwanda ni wengi sana wanaokuja kufanya biashara hii huku ikisemekana kuwa hawana vibali vya kuishi na vya kufanya Biashara hiyo ya madini hayo hapa nchini”, Alisema Wabulungu Haruna mchimbaji wa eneo hilo.

Kwa upande wake Afisa Madini Mkoa wa Kagera Arbogasti Kalist alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya Suala hilo alisema kuwa kweli Madini ya Bati yapo katika eneo hilo lakini hakuna mtanzania yeyote liyejitokeza katika kuomba kibali cha kufanya shughuli za uchimbaji katika maeneo hayo.

“Pia ndugu Mwandishi Watanzania katika madini hayo waanatumika kama Madalali tuu kwa kuwa hapa nchini hakuna mitambo ya kuchenjua madini hayo na hivyo hali ambayo Wanyarwanda wana mashine hizo na kufanya biashara hiyo kuendeshwa na Wanyarwanda kutoka nchi ya jirani”, Alisema Afisa Madini huyo.

Pia alisema kuwa kuwa kuhusu majengo hayo ya Serikali kupangishwa Wanayarwanda Afisa Madini huyo alisema kuwa baada ya Kampuni ya Stamico kuondoka waliona kuwa majengo hayo yasibaki wazi na hivyo kuamua kuyapangisha Wananchi walipo katika eneo hilo wakiwemo Wanyarwanda hao.

Katika suala la Risiti Afisa huyo alisema kuwa waliingia mkataba na Kijiji kwa lengo la kugawana mapato yanayotokana na ushuru wa wachimbaji huku stakabdhi hizi feki zikiwa na mihuri inayooesha imegongwa kutoka katika ofisi za Madini za Mkoa.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply